Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Hamad Hassan Chande (kulia), akutana na Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa Nchini Sweden Mhe. Janine Alm Erickson kujadili maeneo ya ushirikiano kati ya Sweden na Tanzania katika masuala ya Mabadiliko ya Tabia Nchi, Nishati jadidifu pamoja na uchumi wa blue. Kikao hicho kimefanyika leo 28/5/ 2021 katika Ofisi ya Makamu wa Rais Jijini Dar es salaam na kimehudhuriwa na Balozi wa Sweden Anders Sjoberg, maafisa kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais na NEMC.
Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa Sweden Mhe. Janine Alm Erickson, akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili Ofisi wa Makamu wa Rais Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Hamad Hassan Chande (katikati), akiwa katika picha ya Pamoja na Mhe. Janine Alm Erickson (kushoto) Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa Sweden, Balozi wa Sweden Nchini Tanzania Anders Sjoberg (kulia) pamoja na Maafisa wa NEMC.