Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa maonyesho ya pili ya elimu ya mafunzo na ufundi yaliyoandaliwa na NACTE kwa kushirikiana na Taasisi ya sekta binafsi (TPSF) kwa lengo kuonyesha bidhaa za elimu ya ufundi, maonyesho yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa,akisisitiza jambo kwa washiriki wakati wa uzinduzi wa maonyesho ya pili ya elimu ya mafunzo na ufundi yaliyoandaliwa na NACTE kwa kushirikiana na Taasisi ya sekta binafsi (TPSF) kwa lengo kuonyesha bidhaa za elimu ya ufundi, maonyesho yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akizungumza wakati wa uzinduzi wa maonyesho ya pili ya elimu ya mafunzo na ufundi yaliyoandaliwa na NACTE kwa kushirikiana na Taasisi ya sekta binafsi (TPSF) kwa lengo kuonyesha bidhaa za elimu ya ufundi, maonyesho yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi NACTE John Kondoro, akizungumza wakati wa uzinduzi wa maonyesho ya pili ya elimu ya mafunzo na ufundi yaliyoandaliwa na NACTE kwa kushirikiana na Taasisi ya sekta binafsi (TPSF) kwa lengo kuonyesha bidhaa za elimu ya ufundi, maonyesho yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akikagua baadhi ya mabanda ya maonyesho kabla ya uzinduzi wa maonyesho ya pili ya elimu ya mafunzo na ufundi yaliyoandaliwa na NACTE kwa kushirikiana na Taasisi ya sekta binafsi (TPSF) kwa lengo kuonyesha bidhaa za elimu ya ufundi, maonyesho yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt .Adolf Rutayuga, akizungumza wakati wa uzinduzi wa maonyesho ya pili ya elimu ya mafunzo na ufundi yaliyoandaliwa na NACTE kwa kushirikiana na Taasisi ya sekta binafsi (TPSF) kwa lengo kuonyesha bidhaa za elimu ya ufundi, maonyesho yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Antony Mtaka akizungumza wakati wa uzinduzi wa maonyesho ya pili ya elimu ya mafunzo na ufundi yaliyoandaliwa na NACTE kwa kushirikiana na Taasisi ya sekta binafsi (TPSF) kwa lengo kuonyesha bidhaa za elimu ya ufundi, maonyesho yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Baadhi ya washiriki na wananchi waliohudhuria uzinduzi wa maonyesho ya pili ya elimu ya ufundi yaliyozinduliwa leo Jijini Dodoma na yanafanyika katika uwanja wa Jamhuri Dodoma kwa siku 7
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa wa pili kutoka kushoto waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau mara baada ya uzinduzi wa maonyesho ya pili ya elimu ya ufundi yaliyozinduliwa leo Jijini Dodoma na yanafanyika katika uwanja wa Jamhuri Dodoma kwa siku 7.
………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
WAZIRI Mkuu,Kassim Majaliwa ametoa wito kwa vyuo nchini kutoa elimu bora inayozingatia viwango vya ubora na vyenye kukidhi mahitaji ya soko ya ajira la sasa na lijalo.
Majaliwa ametoa kauli hiyo leo Mei 28,2021 jijini Dodoma wakati akifungua maonyesho ya pili ya elimu ya ufundi yaliyoandaliwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) jijini Dodoma.
Waziri Mkuu amesema kuwa ubunifu aliouona katika maonyesho hayo ukiendelezwa na kuongeza uzalishaji unaweza kukidhi mahitaji ya soko la ndani na nje .
“Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025 imeweka wazi kuwa elimu ni kipaumbele cha juu kwani ndiyo kitovu cha kuleta mabadiliko ya kiuchumi kwenye jamii”.
Pia Majaliwa amesema kuwa vyuo vinapaswa kutumia fursa ya maonesho hayo kujitathmini na kujipima ili kuona ni kwa namna gani vinaweza kutoa Elimu na Mafunzo ya Ufundi bora yanayokidhi mahitaji ya sasa ya soko la ajira na kutoa fursa kwa vijana kujiajiri.
“Vyuo na taasisi zinazotoa elimu hii ni lazima vihakikishe vinatoa elimu bora inayokidhi viwango na mahitaji ya soko la sasa la ajira”
Waziri Majaliwa amesema kuwa Serikali itaendelea kuweka sera nzuri zinazotoa fursa kwa Vyuo vya ufundi na sekta binafsi ili kuhakikisha mafanikio yanapatikana huku akiitaka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kuimarisha ushirikiano kati ya sekta binafsi ili kukuza ujuzi huo.
“Serikali inatambua na kuthamini mchango mkubwa unaotolewa na taasisi za umma na binafsi ambazo zinatoa Elimu na Mafunzo ya Ufundi hapa nchini. Hivyo, natoa wito kwa wadau wote kuungana na Serikali kuwekeza katika utoaji wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi katika fani mbalimbali”
Vilevile, ameitaka sekta binafsi nchini inapokutana na changamoto yoyote kufika Serikali ili waweze kufanya kazi kama timu na kukabiliana changamoto hiyo ya ajira.
Waziri Mkuu ,ametoa wito kwa wadau wote kuendelea kushikamana, kuzungumza lugha moja kwa kuhakikisha mwelekeo huo unaeleweka kwa Watanzania.
Kwa upande wake,Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amesema kupitia maonyesho hayo wadau wataweza kubadilishana mawazo ya nini kifanyike katika kuboresha utoaji wa elimu ya ufundi hapa nchini.
“Tutaweza kukuza mashirikiano katika kuhakikisha vijana wanapata sehemu za kwenda kufanya mafunzo kwa vitendo.Serikali inatambua umuhimu wa elimu inayozingatia ujuzi na umahiri kwa vijana wetu katika kufanikisha mageuzi ya uchumi hapa nchini,”amesema.
Awali, Mwenyekiti wa baraza la uongozi NACTE, Prof.John Kondoro, amesema NACTE itaendelea kwa juhudi kubwa kusimamia utoaji wa mafunzo na kuhakikisha elimu ya ufundi inatolewa kwa ubora unaotakiwa ili iweze kukidhi mahitaji ya soko la ajira la ndani.
Amesema mitaala ya umahiri inayotolewa na vyuo vya elimu ya mafunzo ya ufundi inawawezesha wanafunzi kujifunza kwa vitendo zaidi na sio nadharia.
“Tatizo kubwa linalovikabili vyuo vyetu ni ukosefu wa nafasi za mafunzo kwa vitendo.Ukosefu huo unasababishwa na ushiriki mdogo wa wadau katika utoaji wa mafunzo na kwamba inatoka na wadau kutotilia maanani ushiriki wao katika utoaji wa mafunzo,”amesema.
Amesema changamoto hiyo inatokana na baadhi ya wanafunzi kushindwa kumudu gharama za mafunzo hayo.