*****************************
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA
Jiji la Arusha la jipanga kutokomeza uchafu na kuboresha usafi wa mazingira kwa kufanya usafi kila siku ya jumamosi ambapo eameanza kufanya kwenye mito na jumamosi ya tarehe 29 wanatarajia kufanya usafi mto Naura.
Akizungumza na waandishi wa habari Meya wa halmashauri hiyo Maxmilian Irange amlisema kuea wanatarajia zaidi ya wakazi 1500 wa jiji la Arusha watashiriki zoezi la ufanyaji usafi pamoja na upandaji wa miti katika chanzo cha maji cha mto Naura.
Meya huyo alisema kuwa zoezi hilo lina kauli mbiu isemayo “Utalii wa ndani unaanza na mimi,unaanza na wewe, unaanza na sisi”,ni rasmi na baraza la madiwani limeridhia na kila diwani ataenda kuhamasisha usafi katika kata yake na hatimaye kuweza kufikia lengo.
Alisema kuwa pamoja na mafanikio ambayo wameyapata tangu zoezi hilo lilipoanza,katika awamu hii wanatarajia kupanda miti kwenye mto Naura upande wa Kata ya Daraja mbili ili kutengeneza mandhari ya jiji la Arusha kuwa mazuri na kupata Arusha ya kijani.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Kamati ya mipango miji,ujenzi na mazingira jiji la Arusha, Naboth Silas ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Lemara alisema wamejipanga kama jiji kuhakikisha mji unakuwa safi na kuwa katika mazingira rafiki kwa ajili ya utalii wa ndani.
Naye Diwani wa kata ya Unga limited na mjumbe wa kamati hiyo Mahamod Said Omary alimpongeza Meya wa halmashauri hiyo kwa hatua aliyoifanya ya kuhakikisha wakazi wa jiji la Arusha wanafanya usafi na kupanda miti.