Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Binilith Mahenge, akizungumza na viongozi wa dini mkoani hapa kwa mara ya kwanza tangu ahamishiwe akitokea mkoani Dodoma katika kikao kilicho fanyika leo Kulia ni .Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhandisi Pascas Muragili na Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dkt. Angelina Lutambi.
Padre Thomas Mangi wa Kanisa Katoliki (RC)
Viongozi wa dini wakiwa kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Viongozi wa dini wakiwa kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea..
Kikao kikiendelea.
Viongozi wa dini wakiwa kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Viongozi wa dini wakiwa kwenye kikao hicho.
Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Waisalaamu (BAKWATA) Manispaa ya Singida, Hamisi Kisuke, akizungumza kwenye kikao hicho.
|
Kaimu Sheikhe wa Mkoa wa Singida, Issa Nassoro, akizungumza kwenye kikao hicho.
Katibu wa Baraza Kuu la Waisalaamu (BAKWATA) Mkoa wa Singida, Sheikhe, Burhani Mlau, akizungumza kwenye kikao hicho.
Mchungaji Wilson Mkoma kuoka Kanisa la EAGT, akizungumza kwenye kikao hicho.
Jaji Mstaafu, Fatuma Masengi,akizungumza kwenye kikao hicho.
Kasisi Joseph Kense wa Kanisa la Anglikana, akizungumza kwenye kikao hicho.
Abdurahaman Hassan Naibu Amri wa Mkoa Jamaat Ansaari Sunna, akizungumza kwenye kikao hicho.
Godwin Myovela na Dotto Mwaibale, Singida.
MKUU wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge amekutana na kufanya mazungumzo na Viongozi wa Dini mbalimbali, ambapo pamoja na kuwaomba ushirikiano, alitumia jukwaa hilo kueleza mipango, mikakati na mwelekeo wa singida mpya katika muktadha chanya wa maendeleo.
Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika ofisini kwake mkoani hapa, Dkt. Mahenge pamoja na mambo mengine, aliwataka viongozi hao wa dini kumpa ushirikiano wa kutosha hususani kwenye eneo la kuongeza tija ya kilimo cha alizeti ili kuokoa fedha nyingi zinazotumiwa na serikali kuagiza mafuta ya kula nje ya nchi.
“Nadhani tuanze na mkakati wa haraka wa kushusha gharama ya mbegu ya alizeti. Mbegu zinazozaa vizuri na kutoa mafuta mengi bei yake haikamatiki ipo juu sana,” alisema Mkuu wa Mkoa.
Akifafanua hilo, alisema kama serikali na wadau watashirikiana katika kushusha gharama ya mbegu hiyo basi ni dhahiri mkoa huo ambao jiografia yake ni rafiki kwa zao hilo itakuwa ni jawabu la kupunguza au kumaliza kabisa changamoto iliyopo ya upungufu wa mafuta ya kula.
Alisema kwa sasa nchi inaagiza takribani Tani laki 5 za mafuta ya kula kila mwaka jambo linalogharimu na kuleta mtikisiko wa uchumi, na alisisitiza katika kuepusha hilo lisiendelee mkoa wa Singida haukwepeki.
“Naomba viongozi wangu wa dini mtuunge mkono nguvu kubwa ielekezwe kwenye ongezeko la uzalishaji wa alizeti,..sababu soko la mafuta ya kula ni la uhakika, na viwanda tunavyo vya kutosha. Suala la hii changamoto ya mbegu na agronomia tunaendelea kushughulika nayo kama mkoa ili kuwezesha viwanda kuwa na malighafi ya kutosha,” alisema Dkt. Mahenge.
Hata hivyo alipongeza juhudi kubwa za aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo, Dkt. Rehema Nchimbi kwa namna alivyosimamia uzalishaji wa zao la korosho na ameahidi kuendeleza zaidi zao hilo kwa ustawi wa uchumi wa wana-singida.
Katika hilo, Mkuu huyo wa Mkoa alihamasisha jamii kujenga utamaduni wa kula vyakula vinavyozalishwa ndani ya nchi ikiwemo korosho, dengu na ufuta ili kupanua zaidi wigo wa soko la ndani kuliko kutegemea soko la nje.
Awali, wakichangia hotuba yake kwa nyakati tofauti, mbali ya kupongeza mkakati mzuri wa serikali uliopo, hususani kwenye eneo la ongezeko la tija ya zao la alizeti, jukwaa hilo lilimsihi Dkt. Mahenge kuweka mkazo katika kuimarisha huduma za afya, ikiwemo ujenzi wa vituo vya afya, ukosefu wa dawa hospitalini, sanjari na kupandisha zaidi ufaulu kwenye sekta ya elimu.
Aidha, walimtaka aharakishe umaliziaji wa miradi ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa iliyopo, Stendi Kuu ya abiria, umeme, maji na miundombinu ya barabara ambayo kasi yake sio ya kuridhisha na imegeuka kero kwa wananchi.
Pamoja na mambo mengine, walimtaka afuatilie serikalini kujua nini hasa kimekwamisha ujenzi wa Uwanja wa Ndege Singida, mkoa ambao ni wa kimkakati na upo jirani zaidi na makao makuu ya nchi huku tayari hatua za usanifu na upembuzi yakinifu kabla ya kuanza ujenzi wa Uwanja huo vilikwishafanyika.