TIMU ya Villarreal ya Hispania imefanikiwa kutwaa taji la UEFA Europa League baada ya ushindi wa penalti 11-10 dhidi ya Manchester United ya England kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 120 Uwanja wa Energa Jijini Gdańsk, Poland.
Gerard Moreno alianza kuifungia Villarreal dakika ya 29 akimalizia pasi ya Dani Parejo, kabla ya Edinson Cavani kuisawazishia Man United dakika ya 55 akimalizia pasi ya Scott McTominay.
Waliofunga penalti za Villarreal ni Gerard Moreno, Dani Raba, Paco Alcácer, Alberto Moreno, Dani Parejo, Moi Gómez, Fred, Francis Coquelin, Mario Gaspar, Paul Torres na kipa Gerónimo Rulli.
Na Man United zilifungwa na Juan Mata, Alex Telles, Bruno Fernandes, Marcus Rashford, Edinson Cavani, Albiol, Daniel James, Luke Shaw, Axel Tuanzebe na Victor Lindelof, wakati David de Gea alikosa mkwaju wake ukipanguliwa na kipa mwenzake, Rulli. PICHA ZAIDI SOMA HAPA