Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana, Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, akizungumza wakati akifungua kongamano la wadau wa elimu ya ufundi lililoandaliwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) lililofanyika leo Mei 27,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana, Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, akifafanua jambo kwa washiriki wa kongamano la wadau wa elimu ya ufundi lililoandaliwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) lililofanyika leo Mei 27,2021 jijini Dodoma.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt .Adolf Rutayuga,akizungumza wakati wa kongamano la wadau wa elimu ya ufundi lililoandaliwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) lililofanyika leo Mei 27,2021 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi NACTE John Kondoro,akizungumza wakati wa kongamano la wadau wa elimu ya ufundi lililoandaliwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) lililofanyika leo Mei 27,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana, Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa kongamano la wadau wa elimu ya ufundi lililoandaliwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) lililofanyika leo Mei 27,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana, Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama,akiwa katika picha za pamoja mara baada ya kufungua kongamano la wadau wa elimu ya ufundi lililoandaliwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) lililofanyika leo Mei 27,2021 jijini Dodoma.
……………………………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Katika kuhakikisha elimu ya ufundi inaboreshwa hapa nchini,Serikali inatarajia kufanya tafiti kubwa mbili ambazo zitaleta majawabu ya namna bora ya kuboresha elimu ya ufundi ili kuendana na soko la ajira na kukuza ujuzi.
Hayo yamebainishwa leo Mei 27,2021 jijini Dodoma na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana, Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama, wakati akifungua kongamano la wadau wa elimu ya ufundi lililoandaliwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF).
Ambapo amesema mwaka huu serikali itahakikisha inafanya tafiti ambazo zitakazoleta tija katika kuboresha elimu ya ufundi na pia kuwa na takwimu za nguvu kazi na ujuzi ulipo nchini, amezitaja tafiti hizo kuwa ni pamoja na kuangalia hali ya nguvu kazi iliyopo kama wanaajirika katika soko la ajira na hali ya rasilimali watu iliyopo nchini na ujuzi wao.
“Huu utafiti tumelenga kuangalia hali ya nguvu kazi tuliyo nayo na tunaamini itasaidia kujua ni asilimia ngapi ya vijana wetu wanaweza kuajirika katika soko la ajira tulionao, sekta zipi zina fursa zipi zaidi kwenye soko la ajira ili kufundisha ufundi unaoendana na mahitaji yaliyopo kwa taifa tusipofanya utafiti huo tutashindwa kuendelea mbele,” amesema Waziri Jenista.
“katika kuangalia hali ya rasilimali watu iliyopo nchini na ujuzi wao, hii itatusaidia kufahamu watanzania waliopo ndani na nje ya nchi wanafananaje na mahitaji yaliyopo kwasasa nini kiongezwe” amesema.
Amesema wameanza kushughulikia vibali vya wageni, kukusanya takwimu kwanini wawekezaji wanataka kuleta wataalamu wakati watanzania wana viwango hivyo, itasaidia kujua ni maeneo gani kuna upungufu wa ujuzi ili kusaidia katika kupanga mipango ya mafunzo hapa nchini.
Pia amewahamasisha wadau wa sekta binafsi kufungua vyuo vingi vya sayansi na teknolojia ili kusaidia kuwa na nguvu kazi yenye ufundi wa kutosheleza mahitaji nchini na kueleza vikwazo ambavyo serikali itaviondoa ili kufanikisha hilo kusaidia kuwa na vyuo vingi hapa nchini vinavyozalisha wataalamu mbalimbali.
“Sisi serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan tumekubaliana tunataka kutumia sekta binafsi kuwa sehemu ya uchumi wa nchi, hatuwezi kujenga vyuo vyote ni muhimu sekta binafsi kusaidia ili kuzalisha nguvu kazi itakayotumika kwenye miradi yetu ya kimkakati,”amesema.
“Kongamano hili mliamua kuliandaa kwa ushirikiano kati ya NACTE na TPSF, nawapongeza kwa kuwakutanisha hapa na TPSF ndio mwajiri anayebeba watu wanaozalishwa kwenye ufundi, tunaamini kupitia kongamano hili mtajadili nini kifanyike kuboresha sekta hii” amesema.
Amesema kuna miradi mingi serikali inatekeleza na katika miradi hiyo baada ya kukamilika inahitaji nguvu kazi ya wataalamu wanaotokana na elimu ya ufundi.
“Tunatakiwa kujiuliza na tukiondoka hapa yawe ni maswali ya kujiuliza, tuna nguvu kazi ambayo itatakiwa kwenye mradi wa bomba la mafuta, watahitajika wenye fani zipi, pia tunazalisha wahitimu wengi nani ana takwimu kujua wameajiriwa wapi, na je wanatosheleza mahitaji ya soko,” amesema.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dkt. Adolf Rutayuga, amebainisha kuwa pamoja na kuwapo kwa kongamano hilo kutakuwa maonesho ya pili ya elimu ya mafunzo ya ufundi ambayo yanatarajiwa kufunguliwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ikiwa ni katika kukuza ujuzi hapa nchini.