Meneja
Urasimishaji Ardhi Vijijini wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (Mkurabita), Anthony Temu (wa pili kulia) akiwaelekeza maafisa wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, jinsi ya kujaza dodoso kwa kutumia mfumo wa ukusanyaji taarifa kwenye simu janja alipofanya nao kikao cha maandalizi ya kwenda kutoa mafunzo ya kuijengea uwezo jamii ya wafugaji katika Kitongoji cha Mogelo wilayani humo. Kutoka kushoto ni Afisa Mifugo, Abbas Mubanga, Afisa Kilimo, Issa Mwambela na Afisa Ushirika, Grace Samwel.
Afisa Kilimo wa Halmashauri hiyo, Abbas Mubanga akichangia mawazo wakati wa kikao hicho. Kulia ni Afisa Ardhi, Anthony Mashilingi.
Temu akijadiliana jambo na maafisa hao.
Afisa Ardhi, Mashilingi akichangia hoja wakati wa kikao hicho cha maandalizi.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mogelo, Talas Taikoo akielezea namna Hati miliki za Kimila zilivyoinufaisha baadhi ya jamii ya wafugaji kwa kuzitumia kama dhamana kukopa fedha benki zilizowasaidia kununua mashamba kwa ajili ya kilimo na kusomesha watoto wao.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mogelo, Taikoo (kulia), akiwa akizungumza na Meneja Urasimishaji Ardhi Vijijini, Temu pamoja na Afisa Ardhi, Mashilingi alipotembelewa nyumbani kwake Mogelo kwa lengo la kupanga maandalizi ya mafunzo hayo.
Temu akiwa ofisini kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mbarali, Kivuma Msangi ambapo alijitambulisha
na kumueleza jinsi mafunzo hayo yatakavyoendeshwa na kuinufaisha jamii
hiyo ya wafugaji.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
wafugaji ambao wengi wao ni wamasai kupatiwa mafunzo na Mpango wa
Kurasimisha Rasilimali na Biashara wa Wanyonge Tanzania (MKURABITA) ya
kuwajengea uwezo kiuchumi jinsi ya kuboresha mifugo yao na kilimo kwa
kutumia hati miliki za kimila kama dhamana kukopea fedha benki na
taasisi zingine za kifedha.
wakati wa kikao cha maandalizi ya mafunzo hayo, kilichohudhuriwa na
maafisa wa Halmashauri ya Wilaya Mbarali, mkoani Mbeya, Meneja
Urasimishaji Ardhi Vijijini wa Mkurabita, Anthony Temu amesema mafunzo
hayo yanafanyika katika Kitongoji cha jamii ya wafugaji cha Mogelo kesho
Mei 27,2021.
mafunzo watakayopatiwa kuwa ni; kuboresha mifugo yao, Kanuni za kilimo
bora, kuthaminisha mali zao, jinsi ya kutunza kumbukumbu za mahesabu,
faida za ushirika, kuchangamkia fursa mbalimbali ikiwemo mikopo kwa
kutumia hati miliki za kimila kama dhamana, faida za kujiunga na mabenki
kwa ajili ya mikopo na ufugaji bora wa nyuki wa asali.
ya kikao na maofisa hao, Temu alikutana na Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, Kivuma Msangi ambapo alijitambulisha
na kumueleza jinsi mafunzo hayo yatakavyoendeshwa na kuinufaisha jamii
hiyo ya wafugaji.
Mdau,
nakuomba uendelee kusikiliza clip hii ya video ujue kilichozungumzwa kuhusu maandalizi
ya mafunzo hayo yatakayohudhuriwa na zaidi ya kaya 60 za jamii ya wafugaji……