Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Bw. Emmanuel Tutuba na Bi. Nnenna Nwabufo, Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Kanda ya AfrikaMashariki, wakisaini mikataba miwili ya mkopo wenye thamani ya dola za Marekani milioni 140 (takriban shilingi bilioni 323.4) kwa ajili ya kufadhili Mradi wa kufua Umeme wa Mto Malagarasi, Jijini Dar es Salaam. Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Bw. Emmanuel Tutuba (kulia), na Bi. Nnenna Nwabufo, Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Kanda ya Afrika Mashariki, wakibadilishana hati za mikataba miwili ya mkopo wenye thamani ya dola za Marekani milioni 140 (takriban shilingi bilioni 323.39) kwa ajili ya kufadhili Mradi wa kufua Umeme wa Malagarasi, katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Bw. Emmanuel Tutuba na Bi. Nnenna Nwabufo, Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa Kanda ya Afrika Mashariki, wakionesha hati za mikataba ya mkopo wa dola za Marekani milioni 140 (takriban shilingi bilioni 323.39) kwa ajili ya kufadhili Mradi wa kufua Umeme wa Malagarasi, hafla hiyo iliyofanyika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Bw. Emmanuel Tutuba, akizungumza wakati wa halfa ya utiaji saini hati za mikataba ya mkopo wa dola za Marekani milioni 140 (takriban shilingi bilioni 323.39) kwa ajili ya kufadhili Mradi wa kufua Umeme wa Malagarasi, hafla hiyo ilifanyika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa Kanda ya Afrika Mashariki Bi. Nnenna Nwabufo, akizungumza wakati wa halfa ya utiaji saini hati za mikataba ya mkopo wa dola za Marekani milioni 140 (takriban shilingi bilioni 323.39) kwa ajili ya kufadhili Mradi wa kufua Umeme wa Malagarasi, hafla hiyo ilifanyika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Jijini Dar es Salaam.
Ujumbe kutoka Tanzania ukiongozwa na Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Bw. Emmanuel Tutuba (wa pili kulia walioketi), wakiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika ukiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa Kanda ya Afrika Mashariki, Bi. Nnenna Nwabufo (wa tatu kulia walioketi), baada ya hafla ya utiaji saini hati za mikataba ya mkopo wa dola za Marekani milioni 140 (takriban shilingi bilioni 323.39) kwa ajili ya kufadhili Mradi wa kufua Umeme wa Malagarasi, katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Jijini Dar es Salaam.
………………………………………………………………………….
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania imeingia mikataba miwili ya mkopo na Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) wenye thamani ya dola za Marekani Milioni 140 kwaajili ya kufadhili mradi wa kufua umeme wa malagarasi.
Akizungumza mara baada ya hafla hiyo iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Mhe.Emmanuel Tutuba amesema kuwa kati ya fedha hizo,dola za Marekani Milioni 120 zitatolewa kupitia dirisha la banki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) na dola za Marekani milioni 20 kupitia Afrika crowing Together Fund.
“Kusainiwa kwa mikataba hii kutaongeza kiwango cha fedha kilichotengwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika kwaajili ya kufadhili miradi ya Sekta ya nishati nchini Tanzania kutoka takribani dola za Marekani Milioni 325.19 hadi kufikia dola za Marekani Milioni 465.19 (takribani shilingi trilioni 1.07). Amesema Mhe.Tutuba.
Aidha Mhe.Tutuba amesema kuwa Benki ya Maendeleo ya Afrika imeonesha nia ya kufadhili mradi mwingine wa kufua umeme wa Kakono utakaokuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 87MW ambapo maandalizi yanaendelea vizuri.
Amesema mradi wa Malagarasi utahusisha ujenzi wa kituo kipya cha uzalishaji wa umeme wa gridi ya 49.5 MW chenye uwezo wa kuzalisha wastani wa GWh 181 za umeme kwa mwaka.
“Utekelezaji wa mradi unalenga kuboresha usambazaji wa umeme katika mikoa ya magharibi mwa Tanzania ili kuchangia mabadiliko ya kijamii na kiuchumi hapa nchini na kusaidia katika jitihada za kupunguza umaskini”. Amesema Mhe.Tutuba.
Hata hivyo amesema mradi huo utapunguza utegemezi wa uzalishaji wa umeme kwa kutumia mafuta mazito na kupunguza upotevu wakati wa umeme.