Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Prof Bernadeta Kilian akizungumzakatika hafla ya kuwapatia vifaa vya kufundishia walimu wa sayansi kwa shule za sekondari.Hafla hiyo jana imefanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Prof Bernadeta Kilian akimkabidhi mmoja wa walimu wa shule za sekondari darubini (Microscope) kufundishia somo la sayansi. Hafla hiyo jana imefanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Prof Bernadeta Kilian akimkabidhi mmoja wa walimu wa shule za sekondari vifaa vya kufundishia somo la sayansi.Hafla hiyo jana imefanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Ras ndaki ya Sayansi asilia na matumizi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof..Thomas Lyimo hafla ya kuwapatia vifaa vya kufundishia walimu wa sayansi kwa shule za sekondari.Hafla hiyo jana imefanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Mkuu wa idara ya zoolojia na wanyamapori Prof. Flora Magige akizungumza katika hafla ya kuwapatia vifaa vya kufundishia walimu wa sayansi kwa shule za sekondari.Hafla hiyo jana imefanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Wadau mbalimbali wa tafiti wakiwa katika hafla ya kuwapatia vifaa vya kufundishia walimu wa sayansi kwa shule za sekondari.Hafla hiyo jana imefanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
*******************************
NA EMMANUEL MBATILO
Walimu wa sayansi wanaofundisha shule za sekondari zilizopo karibu na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani wameudhuria mafunzo ya matumizi ya darubini (microscope) na ukusanyaji na utunzaji wa sampuli ili kuwarahisisha katika ufundishaji wao mashuleni.
Akizungumza jana na waandishi wa habari katika hafla hiyo Jijini Dar es Salaam Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof Bernadeta Kilian ameiomba ndaki ya sayansi ya Chuo hicho kutumia mradi huo kuongeza idadi ya wanawake katika somo la sayansi mashuleni.
Aidha Prof,Kiliani alisema kupitia mradi huo ameitaka ndakihiyo kutumia tafiti za kidigitali kutatuachangamoto za ufaulu wa sayansi mashuleni ili kuweza kuzalisha wahandisi wengi nchini.
Nae Ras ndaki ya Sayansi asilia na matumizi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof..Thomas Lyimo alisema kutokana na ufaulu mdogo katika shule za kata waliamua kuunda mkakati ambao wameanza kuutekeleza wakuweza kushiriki kutoa tatizo kubwa ambalo linazikumba shule za kata ili ufaulu wake ufikie mkubwa.
“Tumeangalia miaka miwili iliyopita hisabati wanafunzi waliofeli ni asilimia 80 katika shule zetu za sekondari na ukienda kwenye masomo mengine kama biology,Chemistry na Phyisics pia wanafeli lakini sio kwa kiwango cha hisabati”. Amesema Prof.Lyimo.