Mkuu wa Wilaya ya Mjini Rashid Simai Msaraka (kulia) akipokea Mwenge wa uhuru kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Maghribi “B” Hamida Mussa Khamis (kushoto) katika Viwanja vya Jeshi (JWTZ) Migombani Mjini Zanzibar
Kiongozi Mkuu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2021 Luteni Josephine Mwambashi (kulia) akipata maelezo kuhusu bwawa la kufugia samaki kwa msimamizi wa mradi wa ufugaji samaki kutoka Baraza la vijana Shehia ya Bitihamrani Abdulhali Khamisi (katikati) wakati mbio za mwenge zilipokagua mradi huo huko kwa Biti Hamrani kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mjini Rashid Simai Msaraka.
************************
Na Khadija Khamis –Maelezo Zanzibar . 23/05/2021
Kiongozi wa Mwenge Luten Joseaphine Paul Mwambashi amewataka vijana kuitumia Teknelojia ya Tehama kwa usahihi na uwajibikaji ili iwaletee faida sio kwa matumizi mabaya ya kuyarejesha nyuma maendeleo ya Taifa .
Akifunga Kongamano la vijana huko Ukumbi wa Rahaleo amesema endapo wataitumia teknelojia hiyo itaweza kuwaletea faida na kupata maendelea chanya kwa Taifa kutokana na kurahisisha upatikanaji wa elimu na malipo katika ukusanyaji wa mapato ya serikali .
Amesema kumekuwa na wimbi kuwa la Vijana wanaojishughulisha na utumiaji wa mtandao kinyume na taratibu kufanya utapeli wa fedha uchochezi udanganjifu,udhalilishaji wa kijinsia pamoja na kusababisha malezi mabaya kwa watoto na vijana
Hivyo ametoa rai kwa vijana kuhakikisha kwamba wanatumia kwa usahihi Teknelojia ya Tehama ili kujenga taifa endelevu na kuweza kupata maendeleo kwa haraka .
Akizungumzia suala zima la mapambano dhidi ya maambukizi ya ukimwi amewataka vijana hao kuepukana na vishawishi vinavyopelekea maambukizi ikiwemo kuachana na tamaa kwani ugonjwa upo katika jamii na inapelekea kupunguza nguvu kazi ya Taifa na kuwashajihisha vijana hao kupima afya zao .
Aidha amesema Mbio za Mwenge zinasisitiza hasa mapambano dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya kwa vijana kwani bado ni tishio jambo ambalo linaathiri nguvu kazi .
Akifahamisha kuwa mbio hizo zinasisitiza mapambano juu ya Ugonjwa wa Malaria ambao huwapata mama wajawazito na watoto hivyo Kiongozi huyo alitoa rai ya kufanya usafi wa mazingira yanayowuzunguka ili kuua mazalio ya mbu pamoja na kutumia vyandarua vilivyoweke dawa .
Hata hivyo wakati Kiongozi wa Mbio za mwenge akizindua mfumo wa kisasa wa teknolojia Msoma Risala Afisa Habari wa Wilaya ya Mjini, Msangu Said amesema katika tathnia hiyo kuna changamoto ya upungufu wa ujuzi kwa vitendo ukosefu wa sera na taratibu ya kuondoa mali ya tehama pamoja na kukosekana kwa wafanyakazi waliofunzwa tathnia hiyo .
alifahamisha kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt . Hussein Ali Mwinyi amekusudia kuijenga Zanzibar mpya kupitia uchumi wa kisasa
( Blue Economy) ambao una mpango mkakati wa kuendeleza wananchi na wafanyakazi kiujumla kuweka ufanisi na kuengeza dhamani katika mfumo wa mazingira ya Tehama.
Kiongozi huyo aliweza kufungua miradi mbali mbali katika Wilaya ya Mjini ikiwemo Mradi wa Ufugaji wa Samaki kwa Vijana wa Shehia ya Bintihamrani ,Mradi wa Maji Chumbuni, ufunguzi wa Studio ya Stone Town na Menginezo .