MENEJA Urasimishaji Rasilimali Ardhi Vijijini wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (Mkurabita), Anthony Temu akiwa na Kaimu Mkuu wa Idara ya Ardhi, Maliasili na Mazingira wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo, Mkoani Iringa, Bernard Kajembe (kushoto) pamoja na Afisa Ardhi wa Halmashauri hiyo, Innocent Ulomi baada ya kufanya kikao na maofisa ardhi cha maandalizi ya kupima mashamba ya wakulima wadogo wa chai 200 kuirasimisha ili wapate hatimiliki za kimila za kuwawezesha kutumika kama dhamana kukopa fedha benki na taasisi zingine za kifedha.
Akizungumza katika kikao cha maandalizi, Temu amesema kwa kuanzia watarasimisha mashamba ya wakulima 200 na kwamba kazi hiyo itakayofanywa na maofisa ardhi wa halmashauri hiyo itavigusa vijiji 5 na kukamilika kwa muda wa siku 14 kuanzia Mei 27, 2021. Vijiji hivyo ni Kidabaga, Ilamba, Lusinga, Magome na Ng’ang’nge.
Naye Kaimu Mkuu wa Idara ya Ardhi, Maliasili na Mazingira wa Halmashauri hiyo, Kajembe amesema kuwa wamejipanga vilivyo na kwamba wana uhakika wataikamilisha kazi hiyo kwa muda uliopangwa.
Temu akiwa katika kikao na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo, Dkt. Lain Kamendu (katikati) akizungumzia maandalizi ya kupima mashamba ya wakulima wadogo wa Chai. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Idara ya Ardhi, Maliasili na Mazingira wa halmashauri hiyo, Bernard Kajembe.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kilolo, Dkt Lain Kamendu.
Temu akiwa katika kikao na maafisa ardhi wa halmashauri hiyo kuzungumzia maandalizi ya kwenda kuwapimia mashamba wakulima 200 katika vijiji vitano wilayani humo.
Baadhi ya maafisa ardhi watakaoshiriki kupima mashamba ya wakulima na kuyapatia hati miliki.
Temu akisisitiza jambo wakati wa kikao hicho. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA