Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani, akizungumza na vyombo vya Habari baada ya wakati wa ziara yake aliyoambatana na Waziri wa Nyumba na Makazi wa Misri, Dkt. Assem El- Gazzar ya kukagua maendeleo na hatua iliyofikiwa katika Ujenzi wa mradi huo, iliyofayika Mei 22, 2021, mkoani Pwani.
Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani,(katikati) na Waziri wa Nyumba na maendeleo ya Makazi wa Misri, Dkt. Assem El- Gazzar wakikagua maendeleo na hatua iliyofikiwa katika Ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme wakati wa ziara yao iliyofayika Mei 22, 2021, mkoani Pwani.
Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani,(kushoto) na Waziri wa Nyumba na maendeleo ya Makazi wa Misri, Dkt. Assem El- Gazzar(kulia) wakiteta jambo wakati wa kikao kabla ya kukagua maendeleo na hatua iliyofikiwa katika Ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme wakati wa ziara yao iliyofayika Mei 22, 2021, mkoani Pwani.
Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani,(katikati) akimuonyesha sehemu ya mradi Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi wa Misri, Dkt. Assem El- Gazzar(kulia) wakati wa kukagua maendeleo na hatua iliyofikiwa katika Ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme wa JNHPP wakati wa ziara yao iliyofayika Mei 22, 2021, mkoani Pwani.
Kaimu kamishna wa umeme na Nishati jadidifu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Innocent Luoga(kulia) na Mwakilishi wa Mhandisi Mkazi wa Mradi wa JNHPP, Mhandisi Lutengano Mwandambo(kushoto),wakizungumza wakati ziara ya kukagua maendeleo na hatua iliyofikiwa katika Ujenzi wa mradi huo iliyofayika Mei 22, 2021, mkoani Pwani.
Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani,(katikati) na Waziri wa Nyumba na maendeleo ya Makazi wa Misri, Dkt. Assem El- Gazzar(kushoto kwa Waziri Dkt. Kalemani ) wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe ulioambata na Waziri wa Misri wakati wa ziara ya kukagua maendeleo na hatua iliyofikiwa katika Ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme wakati wa ziara yao iliyofayika Mei 22, 2021, mkoani Pwani.
Kazi ya ujenzi ikiendelea katika mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere uliopo mkoani PWANI.
……………………………………………………………………………………
Zuena Msuya na Henry Kilasa, Pwani
Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani amewaeleza watanzania kuwa mradi wa kufua Umeme wa Julius Nyerere( JNHPP) utaanza kuzalisha Umeme utakaotumika katika gridi ya taifa kuanzia Mwezi Juni 2022 kwa kuwa hatua ya ujenzi ya maeneo muhimu ya kuzalisha umeme yamefikia 52.8% mpaka sasa.
Dkt. Kalemani alisema hayo wakati wa ziara yake aliyoambatana na Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi wa Misri, Dkt. Assem El- Gazzar ya kukagua maendeleo na hatua iliyofikiwa katika Ujenzi wa mradi huo, iliyofayika Mei 22, 2021, mkoani Pwani.
Dkt. Kalemani alisema kuwa kasi ya Ujenzi wa mradi huo inaendelea vizuri na kwamba watanzania wataanza kunufaika kwa kutumia Umeme unaozalishwa katika bwawa hilo mwezi Juni Mwakani.
Alisema kuwa, katika kukuhakikisha mradi huo unakamilika ndani ama kabla ya muda ulipangwa, amewataka wahandisi wote wa kampuni inayotekeleza mradi huo kuishi ndani ya eneo la mradi ili kufanya kazi hiyo usiku na mchana.
“Ujenzi wa ukuta wa kingo ya kuzuia maji kwenye bwawa unaendelea vizuri, kuanzia Novemba Mwaka huu tutaanza kujaza Maji katika bwawa letu na hadi kufika Aprili mwakani tayari Maji yatakuwa yamejaa kufikia kiwango cha kutosha kuzalisha Umeme, Mwezi Mei, 2022, tutafanya majaribio ya mitambo ya kuzalisha Umeme na Mwezi Juni tutaanza kuzalisha Umeme utakaoingizwa katika Gridi ya taifa kwa matumizi”, alisema Dkt. Kalemani.
Hata hivyo Dkt. Kalemani alieleza kuwa, tayari mashineumba (Transfoma) 6 kati ya 27 zitazotumika kuongezea nguvu ya Umeme pindi utakapoanza kuzalishwa zimeshawasili nchini huku zingine zikiwa mbioni kufika.
Ameiagiza Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) kuwa, ndani ya siku 7 kuanzia sasa ihakikishe inakamilisha taratibu zote za kuwezesha mitambo hiyo kutoka bandarini na kufikishwa katika eneo la mradi ili kuanza kufungwa katika maeneo husika.
Sambamba na hilo, aliieleza kuwa, baadhi ya wataalamu wako nchini China kukagua baadhi ya mitambo mingine inayotengenezwa huko kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa kuzalisha Umeme.
Hivyo amewataka wataalam hao kusimamia kazi hizo kwa umakini mkubwa na kuweka mbele maslahi ya taifa katika kujenga Miradi imara, bora na mikubwa itakayodumu kwa miaka mingi.
Mpaka sasa tayari mkandarasi anayetekeleza mradi huo ameshalipwa kiasi cha shilingi Trilioni 2.43 na fedha hizo zimekuwa zikilipwa kwa wakati.
Aliweka wazi kuwa serikali haitamvumilia yeyote atayejaribu ama kusababisha mradi huo kutokamilika kwa wakati kwa kuwa kila kitu kimekuwa kikitekelezwa kwa kuzingatia misingi ya mkataba, na atakayebainika kufanya hivyo hatua za kisheria zitachuliwa dhidi yake.
Kwa upande wake Waziri wa Nyumba, na Maendeleo ya Makazi wa Misri, Dkt. Assembly El – Gazzar alimuahakikishia Dkt. Kalemani kuwa mradi huo utakamilika ndani ya muda uliopangwa, na kwamba kwa kufanya hivyo kutazidi kuimarisha mahusiano mazuri kati ya nchi hizo mbili.
Dkt. El – Gazzar alisema kuwa watakapokamilisha mradi huo kama ilivyopangwa, nchi yake itakuwa katika nafasi nzuri ya kuendelea kuwekeza Tanzania kwa kupata kazi ya kutekeleza mradi mbalimbali ya maendeleo.
Aidha alisema serikali yake itaendelea kuimarisha usimamizi wa mradi huyo na kwamba watahakikisha watalaam wote wanaotakiwa katika kila hatua ya kutekeleza mradi huo wanafika kwa wakati nchini na kutimiza majukumu yako kama inavyotakiwa.
Dkt. El-Gazzar aliambatana na ujumbe wa watu zaidi ya 50, na hii ikiwa ni mara yake ya nne kutembelea mradi huyo tangu ulipoanza kutekelezwa mwaka 2019, huku Dkt.Kalemani ikiwa ni Mara yake ya 16 kutembelea mradi huyo.