Wakaguzi wa TBS kanda ya ziwa wakiwa katika ukaguzi wa kushtukiza katika viwanda vya kuzalisha mifuko ya sandarusi vilivyopo jijini Mwanza kwa ajili ya kuangalia uzalishaji pamoja na uchukuaji wa sampuli kwa ajili ya kupima maabara kama zimekidhi matakwa ya kiwango husika.
Mkaguzi wa TBS kanda ya ziwa Bw.Donald Mkonyi akiangalia ukomo wa matumizi ya bidhaa katika duka la chakula wakati wa ukaguzi wa bidhaa sokoni katika Halmashauri ya Nyamagana. Wauzaji walisisitizwa kuziondoa sokoni mara moja bidhaa zinapokwisha muda wake wa matumizi kwani zinahatarisha usalama wa afya za walaji.
*************************
Shirika la Viwango Tanzania TBS limeendelea na ukaguzi wa bidhaa kanda ya ziwa ambapo imefanya ukaguzi katika maduka ya chakula pamoja na viwanda vya kuzalisha mifuko ya sandarusi jijini Mwanza.
Wazalishaji wameshauliwa kuzalisha bidhaa zilizokidhi viwango ili kuweza kumlinda mteja, wakati huohuo wauzaji wa bidhaa wametakiwa kuhakikisha wanaziondoa sokoni mara moja bidhaa zinapokwisha muda wake wa matumizi kwani zinahatarisha usalama wa afya za walaji.