Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka leo amekabidhiwa ofisi na aliyekuwa Mkuu wa Idara hiyo, Humphrey Polepole, huku akisisitiza kuwa chama kipo imara.
Makabidhiano ya ofisi hiyo yamefanyika Leo katika ofisi za CCM ofisi Ndogo Lumumba jijini dar es salaam na kuhudhuriwa na baadhi ya viongozi akiwemo mjumbe wa NEC Ernest Sungura ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Uhuru Media Group.
Katika makabidhiano hayo shaka amesema chama Cha mapinduzi bado kipo imara na nitaendelea kuwa imara kutokana na uongozi madhubuti wa mwenyekiti wa CCM Rais Samia Suluhu Hassan.
Kupitia Idara hiyo shaka amesema atatumia weledi wake na uzoefu ndani ya chama katika kuenezi Itikadi ya chama nchi nzima ikiwemo kupata wanachama wapi na kueneza siasa Safi.
Aidha amesema atahakikisha anasikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi kwa kwa kuielekeza serikali itatue kero zitakazojitokeza ili wananchi wawe na Imani na chama pamoja na serikali iliyopo madarakani
Naye Polepole ambaye Sasa ni Mbunge wa kuteuliwa amewaomba waandishi wa habari kumpa ushirikiano Shaka katika kutekeleza majukumu yake mapya ya CCM kupitia Idara ya Uenezi.
Pia amekabidhi Shaka Boksi lililojaa barua za kero za wananchi akimomba kuendelea kuzitafutia ufumbuzi wa kina.