Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Brig. Jen. Dkt. Gabriel Sauli Mhidize, akimtambulisha kwa Wafanyakazi wa MSD, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa ( MSD) Meja Jenerali Gabriel Saul Mhidze, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel, (wa pili kulia) alipokitembea jana kiwanda cha kuzalisha dawa, kinachosimamiwa na Bohari ya dawa (MSD) Keko Pharmaceuticals.
Utambulisho ukiendelea.
Utambulisho ukiendelea.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Molle, akizungumza na Wafanyakazi wa MSD. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa ( MSD) Meja Jenerali Gabriel Saul Mhidze.
Mkutano na Waziri ukiendelea.
Na Mwandishi Wetu
NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel amewapongeza MSD kwa kufufua uzalishaji wa dawa katika kiwanda cha kuzalisha dawa, kinachosimamiwa na Bohari ya dawa (MSD) Keko Pharmaceuticals.
Dkt. Mollel ametoa pongezi hizo alipotembelea kiwanda hicho,katika ziara yake aliyoifanya jana Bohari ya Dawa (MSD) kujionea uzalishaji wa dawa na barakoa unaofanywa na MSD.
Kiwanda cha Keko Pharmaceuticals kinazalisha aina 10 za dawa zikiwemo za maumivu aina mbili na nyingine 8 zikiwa ni dawa za kuua vimelea vya magonjwa ya kuambukiza (antibacteria/antibiotics)
Mwishoni mwa wiki Naibu Waziri huyo atatembelea mradi wa kiwanda kingine cha MSD cha kutengeneza mipira ya mikono, kilichopo Idofi,Makambako mkoani Njombe.