Wajumbe walioshiriki Kikao cha 14 cha Bodi ya Maji ya Taifa kilichofanyika katika makao makuu ya Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Nyasa wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Kikao cha 14 cha Bodi ya Maji ya Taifa kilichofanyika katika makao makuu ya Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Nyasa katika mji wa Tukuyu, wilayani Rungwe, mkoani Mbeya.
Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Maji ya Taifa walioshiriki Kikao cha 14 cha Bodi ya Maji ya Taifa kilichofanyika katika makao makuu ya Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Nyasa katika mji wa Tukuyu, wilayani Rungwe, mkoani Mbeya.
Kikao cha 14 cha Bodi ya Maji ya Taifa kilichofanyika katika makao makuu ya Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Nyasa katika mji wa Tukuyu, wilayani Rungwe, mkoani Mbeya.
……………………………………………………………………………..
Bodi ya Maji ya Taifa imekutana na kujadili hali ya rasilimali za maji nchini kwa kipindi cha mwaka 2017-2019 katika kikao kilichofanyika makao makuu ya Bodi ya Maji ya Bonde la Ziwa Nyasa katika Wilaya ya Rungwe, mkoani Mbeya.
Kikao hicho cha 14 kimekutanisha wajumbe wa Bodi ya Maji Taifa, Maafisa Maji wa Bodi za Maji za Mabonde 9 nchini na wajumbe wa menejimenti wa Wizara ya Maji.
Mkurugenzi wa Rasimali za Maji, Dkt. George Lugomela ambaye pia ni Katibu wa bodi hiyo amesema dhumuni la kikao hicho kilikuwa ni kujadili hali ya rasilimali za maji kwa mabonde yote 9 unaohusisha usimamizi na utunzaji wa rasilimali za maji kwa mustakbali wa maendeleo ya taifa.
Dkt. Lugomela amesema Serikali imechukua hatua kwa kutekeleza mpango maalum wa kusimamia, kutunza na kuendeleza rasilimali za maji ili ziweze kuwa endelevu ziweze kunufaisha taifa kwa miaka mingi.
Akibainisha kuwa mpango huo umelenga kutatua changamoto kubwa ya uvamizi na uharibifu wa vyanzo vya maji inayotokana na shughuli za kibinadamu zinazofanyika kiholela, pamoja na mabadiliko ya tabia nchi hali inayosababisha athari kubwa kwa upande wa rasilimali za maji.
Pia, kikao hicho kimejadili utekelezaji wa shughuli za usimamizi wa rasilimali za maji na kutathmini utendaji wa bodi.
Aidha, Bodi ilifanya ziara ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa shughuli za usimamizi wa rasilimali za maji zinazofanywa katika Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Nyasa wilayani Rungwe na Programu ya Pamoja ya Kuendeleza Bonde la Mto Songwe iliyo chini ya Kamisheni ya Pamoja Kati ya Tanzania na Malawi ya Bonde la Mto Songwe wilayani Kyela.
Bodi imeridhishwa na utekelezaji wa shughuli za usimamizi wa rasilimali za maji ikiwemo kuainisha vyanzo vyote, kuviwekea mipaka, kuvitunza, pamoja na kupima wingi na ubora wa maji hatua ambayo imeleta mafanikio makubwa kwenye vyanzo vingi kikiwemo chanzo cha maji cha Nyibuko na Mto Kiwira walivyotembelea.
Bodi ya Maji ya Taifa ya Maji ni chombo kinachotoa ushauri kwa Waziri wa Maji masuala yanayohusu Sekta ya Maji ikiwemo uendelevu wa rasilimali za maji.