Mhe Mbunge wa Jimbo la Hanang’ Mkoani Manyara, mhandisi Samwel Xaday Hhayuma (kulia) akizungumza na wafanyabiashara wa mazao wa soko la Endagaw alipotembelea leo Mei 22.
********************
Na Mwandishi wetu, Hanang’
MBUNGE wa Jimbo la Hanang’ Mkoani Manyara, Mhe mhandisi Samwel Xaday Hhayuma, leo Mei 22, 2021 amefanya ziara kwenye Kata ya Endagaw na kuzungumza na wafanyabiashara wa mazao katika soko la Afrika Mashariki lililopo Endagaw wilaya ya Hanang’ nakujionia maendeleo ya soko hilo.
Mbunge huyo mhandisi Hhayuma ameahidi kuendeleza viwanda vya usindikaji wa nafaka sokoni hapo ili kuongeza uzalishaji na kuongeza fursa za ajira kwa vijana.
Mbunge huyo Hhayuma ametembelea shule mpya ya Jikomboe na kuchangia saruji mifuko 100 pamoja na bati ili kusaidia umaliziaji wa shule hiyo
Mbunge huyo pia ametembelea eneo la Tindiga ambalo limekuwa na mgogoro wa muda mrefu na kuzungumza na wenyeji wa eneo hilo ili kutatua mgogoro huo.
Mhandisi Samwel Hhayuma ametembelea eneo la Gidangu ambalo kwa muda mrefu kulikuwa na changamoto ya kivuko na kutoa shilingi milioni tano ili kujenga kivuko.