******************************
KUPATIKANA NA MAZAO YA MISITU
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia MOSES JOSEPH [38] Dereva wa Gari namba T.667 AJA Canter Custom, HEZRON KAPOKELA [47] Mkazi wa Mbozi, Mkoa wa Songwe na wenzake 11 kwa tuhuma za kupatikana na mazao ya misitu, viazi pori @ Chikanda.
Watuhumiwa walikamatwa mnamo tarehe 21.05.2021 majira ya saa 05:00 alfajiri huko eneo la Stendi ya Umalila, Mtaa wa DDC – Mbalizi, Kata ya Utengule, Tarafa ya Usongwe, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoa wa Mbeya baada ya Askari Polisi kulikamata Gari namba T.667 AJA aina ya Canter Custom likiendeshwa na dereva MOSES JOSEPH [38] Mkazi wa Uyole kati ikiwa imebeba magunia 23 ya viazi pori @ Chikanda zao la misitu pamoja na wenye viazi hivyo akiwemo HEZRON KAPOKELA [47] Mkazi wa Mbozi, Mkoa wa Songwe na wenzake 11 wakitokea hifadhi ya Kitulo.
KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO].
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia CHRISTINA VANANCE [20] Mkazi wa Mabatini Jijini Mbeya kwa tuhuma za kupatikana na Pombe ya Moshi [Gongo] ujazo wa lita 5.
Mtuhumiwa alikamatwa mnamo tarehe 21.05.2021 majira ya saa 13:00 mchana katika misako inayoendelea maene ya mtaa na Kata ya Mabatini, Tarafa ya Sisimba Jiji na Mkoa wa Mbeya. Mtuhumiwa ni muuzaji na mtumiaji wa Pombe hiyo, atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.
KUINGIZA BIDHAA NCHINI BILA KIBALI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia ROJA ALEX [35] Mkazi Lubele kwa tuhuma za kuingiza nchini sukari katoni 08 kutoka nchini Malawi bila kibali.
Mtuhumiwa alikamatwa mnamo tarehe 21.05.2021 majira ya saa 09:30 asubuhi huko Kitongoji cha Ibungu, Kata ya Ndandalo, Tarafa ya Unyakyusa, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya akitokea nchini Malawi akiwa amebeba sukari hiyo bila kuwa na kibali.
KUKAMATWA WEZI WA PIKIPIKI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia 1. SAMWEL GODFREY @ MWAMBENJA [21] fundi magari, Mkazi wa Kiwira – Tukuyu 2. BRAYTON JOSEPH @ NYANGALI [25] Mkazi wa Iwambi – Mbeya na 3. ABDUL FREDY @ FUMBO [24] Mkazi wa Nzovwe – Mbeya kwa tuhuma za kujihusisha na matukio ya wizi na uporaji wa Pikipiki na kuziuza nchini Malawi.
Watuhumiwa walikamatwa mnamo tarehe 21.05.2021 majira ya saa 13:30 mchana huko Kijiji cha Kasumulu mpakani na Malawi, Kata ya Njisi, Tarafa ya Unyakyusa, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya. Watuhumiwa ni wahalifu wa matukio ya wizi / uporaji wa Pikipiki kwa tuhuma za matukio ya wizi na uporaji wa Pikipiki ambazo baada ya kuziuza hapa nchini huzisafirisha hadi nchini Malawi kupitia vivuko visivyo rasmi hadi Songwe Malawi kwa mtu aitwaye RICHARD NGOMA @ PINDA ambaye uwalipa ujira wa kiasi cha Tshs.120,000/=.
Mtakumbuka mnamo tarehe tarehe 20.05.2021 huko Uyole Jijini Mbeya, Jeshi la Polisi mkoani hapa lilimkamata SAMWEL MWANG’OMBE [46] Mkazi wa Uyole kwa tuhuma za kupatikana na mali ya wizi Bajaji yenye namba za usajili MC.321 CSA aina ya TVS ambayo aliiba hapa nchini na kwenda kuiuza nchini Malawi.
TAARIFA YA KUMATA MALI YA WIZI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limefanikiwa kukamata mali mbalimbali za wizi huko Kijiji cha Mpandapanda, Kata ya Kiwira, Tarafa ya Ukukwe, Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya ambazo ni:-
- TV flat screen 01 Simsung inchi 24,
- Laptop aina ya dell,
- Simu 01 Tecno W4 na remote 03 za Subwoofer.
Mtuhumiwa ambaye anafahamika alikimbia na kutelekeza mali hizo baada ya kuwaona askari wa doria. Mali hizo ziliibwa tarehe 21.05.2021 majira yam chana katika tukio la kuvunja nyumba ya bwana LAZARO HILARY CHENELO. Msako wa kumtafuta mtuhumiwa ambaye ametambulika unaendelea.