………………………………………………………………………
Kampuni ya simu janja za mkononi Infinix ina waletea watumiaji na wapenzi wa simu janja za kampuni yao shindano maridani kubwa litakalo ibua vipaji vya watanznia wote.
Akizungumzia shindano hilo Afisa Mahusiano Infinix Aisha Karupa, amesema kuwa lengo la shindano ni kuwapa nafasi vijana wote kuonesha na kukuza vipaji vyao ndani na nje ya Tanzania na kwa uzuri zaidi kampuni ya infinix haijaweka wigo wowote wakuzuia aina ya kipaji.
Bi. Karupa amesema kuwa watu wataonyesha vipaji vyao kwa ufundi kile wanachoweza kupitia kipaji vyao kama kucheza, kuimba, kutangaza, kuchekesha kuchora na nakadhalika na kujishindia hadi Tsh.5,000,000.
“Kanuni za kushiriki, washiriki wote wanatakiwa kushiriki shindano hili kwa njia ya mtandao wa kijamii Instagram ambapo wanataikiwa kufanya ni Tuma na sambaza video yako ukiwa unaonesha kipaji chako kwenye mtandao wa kijamii instagram” amesema Bi. Karupa.
Ameeleza kuwa wanapaswa kutumia hashtag #10ya10search na kisha tag @infinixmobiletz, shirikisha rafiki zako ili waweze kushiriki nawe kwenye video yako.
Amebainisha kuwa zawadi katika shindano hilo, mshindi wa 1 anapata 4,600,000Tsh, simu janja kutoka infinix na ticket kuhudhulia uzinduzi wa simu mpya ya infinix.
Mshindi wa 2 kuondoka na 2,300,000Tsh, simu janja na ticket ya kuhudhuria uzinduzi wa simu mpya ya Infinix.
Mshindi wa 3 hadi wa 10 kuondoka na 1,150,000Tsh, simu na ticket ya kuhudhuria uzinduzi wa simu mpya ya Infinix.
Mashindano haya kuendeshwa na wasanii maarufu kutoka kwenye tasnia ya Music, utangazaji, comedy na kadhalika tafadhali tembelea @infinixmobiletz kwa mengi zaidi.