Balozi wa Uholanzi hapa nchini Mhe. Jeroen Verheul akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) wakati walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiteta jambo na Balozi wa Uholanzi hapa nchini Mhe. Jeroen Verheul wakati walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Mazungumzo baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) na Balozi wa Uholanzi hapa nchini Mhe. Jeroen Verheul yakiendelea katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Mazungumzo baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) na Balozi wa Uholanzi hapa nchini Mhe. Jeroen Verheul yakiendelea katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) katika picha ya pamoja na Balozi wa Uholanzi hapa nchini Mhe. Jeroen Verheul pamoja na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ulaya na Amerika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Hassan Mwamweta (mwenye tai nyekundu) na maafisa waandamizi kutoka wizarani pamoja na ubalozi wa Uholanzi
***********************************
Na Mwandishi wetu, Dar
Serikali imesema mwamko wa biashara na uwekezaji ni mkubwa kwa sasa baada ya baadhi ya makampuni na taasisi zilizokuwa zimefunga shughuli zao kuanza kurejea na kwamba serikali kwa sasa inapitia upya sera yake ya uwekezaji ili kuweka mazingira bora Zaidi ya biashara na uwekezaji.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula ameyasema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uholanzi hapa nchini Mhe. Jeroen Verheul Jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa tamko la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kuhusu kuimarisha mazingira ya uwekezaji na biashara yanakuwa rafiki.
“Mwamko wa biashara na uwekezaji ni mkubwa kwa sasa baada ya baadhi ya makampuni na taasisi zilizokuwa zimefunga shughuli zao kuanza kurejea na kwamba serikali kwa sasa inapitia upya sera yake ya uwekezaji ili kuweka mazingira bora na salama zaidi ya biashara na uwekezaji,” amesema Balozi Mulamula.
Balozi wa Uholanzi hapa Nchini Mhe Jeroen Verheul amekiri kuwa Tanzania ina fursa na rasilimali nyingi zinazohamasisha na kuvutia biashara na uwekezaji licha ya uwepo wa maeneo machache yanayohitaji maboresho ambayo yakifanyiwa kazi ipasavyo makampuni mengi kutoka Ulaya na mabara mengine yatakuja kuwekeza Nchini.
“Tanzania ina fursa na rasilimali nyingi za uwekezaji licha ya uwepo wa maeneo machache yanayohitaji maboresho ambayo yakifanyiwa kazi ipasavyo kampuni nyingi kutoka Ulaya na mabara mengine na hata hapa Tanzania zitakuja kuwekeza kwa wingi,” amesema Balozi Verheul
Balozi huyo ameongeza kuwa kupitia kauli mbiu ya diplomasia ya uchumi nchi yake iko tayari kushirikiana na Tanzania katika kuangalia maeneo yenye changamoto na kuyatafutia ufumbuzi kwa maslahi ya pande zote mbili.
Katika tukio jingine, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma amekabidhi ofisi kwa Katibu Mkuu mpya Mhe. Joseph Edward Sokoine ambapo tukio hilo limeshuhudiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula.