………………………………………………………………
NJOMBE
Baada ya figisu na sintofahamu ya muda mrefu ya uchaguzi wa Njorefa ,hatimae chama cha mpira wa miguu mkoa wa Njombe kimefanya uchaguzi mkuu na kuwapata viongozi wapya watakaosimamia mpira katika kipindi cha miaka mingine 4 ambapo Thobias Lingalangala ameshinda nafasi ya mwenyekiti kwa kupata kura 18 ambayo ni sawa na asilimia 100 akimdondosha Yono Kevela aliyekuwa anatetea nafasi yake.
Awali akitangaza matokeo msimamizi kuu wa uchaguzi huo Uliohudhuriwa na mwakilishi wa TFF wakili msomi Deogratus Mbisi amemtangaza bwana Lingalangala kuwa mwenyekiti kwa kupata kura zote za wajumbe huku wengine wakiwa ni Obedy Mwakasungula aliyeshinda nafasi ya katibu wa Njorefa,Emmanuel Mbogela makamu mwenyekiti,Evansi Nyinge akichaguliwa kuwa mwakilishi wa TFF huku Lusubilo Mwakafuje akishinda nafasi ya uwakilishi wa vilabu.
Akitoa shukrani kwa wajumbe na vipaumbele anavyokwenda kuanza navyo mwenyekiti wa mpya wa NJOREFA amesema kupata asilimia 100 ya kura za wajumbe ni deni kubwa hivyo anakwenda kuanza na ujenzi wa ofisi ya NJOREFA,Kuvumbua vipaji na kuvitambua vilabu vyote vya mkoa ili kuviwekea mazingira mazuri ya kushiriki ligi zao.
Mara baada ya kuupata uongozi mpya wapenzi wa soka mkoa wa Njombe waliokuwa nje ya ukumbi wa uchaguzi wakisubiri matokeo akiwmeo Solanus Muhagama na Judith Sanga wakatoa hisia zao na matarajio yao kuwa mkoa unakwenda kurejesha heshima uliyopoteza katika soka
Katika uchaguzi huo mwenyekiti aliyekuwa anatetea nafasi yake Yono Kevela hakushiriki uchaguzi