…………………………………………………………………………………
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Waziri wa fedha na mipango Dkt Mwigulu Nchemba anatarajiwa kufungua mkutano wa 26 wa wanahisa wa benki ya CRDB unaotarajiwa kufanyika mei 22 mkoani Arusha katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa{AICC} huku gawiwo la wanahisa likipanda kutoka shilingi17 ya mwaka 2019 na kufikia shilingi 22 kutokana na faida ya bilioni 165 waliyoipata 2020.
Hayo yalisema na mkurugenzi mkuu wa benki hiyo Abdulmajid Nsekela wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na mkutano huo utakaofanyika siku ya jumamosi na siku ya ijumaa tarehe 21 ikiwa ni semina kwa wanahisa hao ambapo alisema kuwa kuwa pamoja na kuwepo kwa janga la Corona mwaka 2020 mwaka huo ulikuwa wa mafanikio kwa benki hiyo kwani walijaribu kupambana na athari za janga hilo kwa kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi na kuweza kupata faida ya shilingi bilioni 165 baada ya kodi jambo ambalo halikuwahi kutukea miaka mingine.
“kila mwaka mkutano mkuu wa wanahisa wa benki yetu unafanyika Mei isipokuwa mwaka jana peke yake ambapo tulifanya mwezi wa sita kutokna na janga la Covid 19 na mwaka huu tunaendelea na ratiba yetu na mkutanoutafanyika tarehe 22 na wanahisa watapata fursa ya kuwa kwenye mkutano moja kwamoja lakini kwa watakao shindwa kufika watashiriki kwa njia ya kidigitali,”Alisema Nsekela.
Alifafanua kuwa gawiwo kwa mwaka huu litapanda kutoka shilingi 17 ya mwaka 2019 na kufikia shilingi 22 kuoka na mafanikio hayo lakini pia mikopo chechefu kwa mwaka 2020 imepungua na kufikia asilimia 4.4 ukilinganisha na na miaka mingine ambapo 2018 ilikuwa asilimia 9 na 2019 ikiwa ni asilimia 5.
“Niwahakikishie wanahisa kuwa benki ina uimara wa kukabiliana na changamoto kwa maana ya kukabiliana na majanga mbalimbali yanayoweza kutokea lakini pia tutaendelea kuhakikisha tunawapa wanahisa wetu taarifa sahihi na kwa wakati,”Alieleza.
Alisema mkutano huo utakuwa na agenda mbalimbali kiwemo Agenda ya kuwachagua wakurugenzi wa bodi ya wanahisa wa wa asilimia 1hadi 10 na wa wanahisa wa chini ya asilimia 1 ambapo alitoa wito kwa wanahisa wa benki hiyo kuhudhuria kwa wingi katika mkutano huo.
Aliendelea kusema kuwa mkutano wa mwaka jana ulikuwa na ubunifu ambao kwa mwaka huu ubunifu huo umeendelea kuongezeka na kwani benki hiyo imekuwepo kwa miaka 24 lakini kila mwaka imekuwa ikijijenga na wanahisa wakiijenga. Na pamoja na mkutano huo mwaka wa 2021 uaendelea ambapo kwa kota ya kwanza wameweza kupata faida ya shilingi milioni 44.