Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na wakuu wa mikoa katika ofisi za Tamisemi mara baada ya kuapishwa kwa wakuu hao leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
*************************************
NA EMMANUEL MBATILO
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Ummy Mwalimu amewataka wakuu wa mikoa kufanya kazi kwa weledi hasa katika ukusanyaji wa mapato bila kutumia mabavu bali kwakusimamia sheria,kanuni na taratibu.
Akizungumza katika kikao na wakuu wa mikoa leo Jijini Dar es Salaam mara baada ya kuapishwa kwa wakuu wa mikoa Mhe.Ummy amesema mapato yamekuwa yakipotea kwasababu hawatumii mifumo ya kieletroniki ya kukusanya fedha wakati mwingine wanakusanya fedha na hawazipeleki benki kabla ya kuanza matumizi.
Amesema watafanya semina na wakuu wa mikoa baada ya wiki mbili ili kuwaonesha maras ile mifumo yote ya usimamizi wa ukusanyaji wa mapato taratibu na vitu gani wanatakiwa kufanya.
“Ninawaomba sana kusimamia na kuongeza nguvu katika kusimamia ukusanyaji wa mapato, tukipata mapato mazuri maana yake tunaenda kutatua kero za maendeleo ikiwemo afya na elimu”. Amesema Waziri Ummy.
Amesema wameleekeza kwenye halmashauri itakayopata bilioni 5 kwenda juu wapeleke asilimia 60 ya mapato yao ya ndani kwenye miradi ya maendeleo na ukipata chini ya bilioni 5 pelkea asilimia 40 kutatua kero za wananchi.
Pamoja na hayo Mhe.Ummya amesema mpaka sasa kuna uhaba wa madawati zaidi ya milioni moja na vyoo vya wanafunzi na walimu hivyo amewataka kwenda kushughulikia changamoto hizo kabla ya shule kuanza kwa muhula januari 2022.
“Tukitumia mapato ya ndani tunmaweza kutatua kero za watanzania na watanzania watafurahi lakini pia tutapata baraka za mwenyezi mungu”. Amesema Waziri Ummy.