Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.
Balozi Liberata Mulamula (Mb) akimkaribisha Balozi wa Pakistan
hapa nchini Mhe. Mohammad Saleem pamoja na ujumbe wake
katika Ofisi ndogo za wizara jijini Dar es Salaam
Balozi wa Pakistan hapa nchini Mhe. Mhe. Mohammad Saleem
akiongea jambo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula katika Ofisi
ndogo za wizara jijini Dar es Salaam
Balozi wa Pakistan hapa nchini Mhe. Mohammad Saleem
akimuonesha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula takwimu za ukuaji wa
biashara kati ya Pakistan na Tanzania katika Ofisi ndogo za
wizara jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.
Balozi Liberata Mulamula (Mb) akimkaribisha Kaimu Balozi wa
Iran hapa nchini Mhe. Hossein Alvandi Behineh katika Ofisi ndogo
za wizara jijini Dar es Salaam
Kaimu Balozi wa Iran hapa nchini Mhe. Hossein Alvandi Behineh
akimuelezea jambo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula katika Ofisi
ndogo za wizara jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.
Balozi Liberata Mulamula (Mb) akimueezea jambo Kaimu Balozi
wa Iran hapa nchini Mhe. Hossein Alvandi Behineh katika Ofisi
ndogo za wizara jijini Dar es Salaam
Kikao kikiendelea
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.
Balozi Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na Balozi wa
Pakistan hapa nchini Mhe. Mohammad Saleem pamoja na baadhi
ya maafisa waandamizi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na
Ubalozi wa Pakistan.
*******************************
Pakistan na Iran zimeahidi kuendelea kuimarisha diplomasia ya uchumi na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa maslahi mapana ya pande zote.
Ahadi hizo zimetolewa kwa nyakati tofauti wakati Mabalozi wa Pakistan na Iran walipokutana kwa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.
Mabalozi waliokutana na Waziri Mulamula ni Balozi wa Pakistani hapa nchini Mhe. Mohammad Saleem pamoja na Kaimu Balozi wa Irani hapa nchini Mhe. Hossein Alvandi Behineh ambapo viongozi hao wamejadili masuala ya kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania na Nchi zao lakini pia kuimarisha na kuboresha diplomasia ya uchumi kwa maslahi mapana ya nchi zote.
Pamoja na mambo mengine, Balozi wa Pakistan Mhe. Saleem ameelezea kufurahishwa na uhusiano mzuri uliopo baina ya Iran na Tanzania na amepongeza hatua mbalimbali ambazo Serikali ya Tanzania imeendelea kuzichukua katika kuimarisha diplomasia ya uchumi.
Nae Kaimu Balozi wa Iran amesisitiza juu ya uwekezaji na biashara ambapo amesema kuwa Serikali yake ipo tayari kufanya biashara na Tanzania na kuinua uchumi wa wananchi wan chi zote mbili.
Kwa upande wake Balozi Liberata Mulamula (Mb) amewahakikishia mazingira salama ya biashara na uwekezaji na kuwaahidi ushirikiano wa kutosha kutoka Tanzania.
Kadhalika,Waziri Mulamula amesema ushirikiano wa diplomasia ya uchumi kati ya Tanzania na Pakistan unatoa fursa nyingi ikiwemo kukuza biashara hasa katika sekta ya kilimo ikiwemo chai, pamba, korosho, mbegu za mafuta, Madini ya Tanzanite, pamoja na uwekezaji.