Na Dotto Mwaibale
WANAFUNZI jijini Arusha wamejengewa uwezo wa kujua Makumbusho ya Taifa katika kilele cha maadhimisho yaliyoadhimishwa duniani kote leo.
Akizungumza na waandishi wa habari katika maadhimisho hayo jijini Mkurugenzi wa Makumbusho ya Viumbe Hai iliyopo jijini Arusha Dkt. Christine Ngereza alisema moja ya shughuli walioifanya ni kuwajengea uwezo wanafunzi wa shule mbalimbali waliofika katika maadhimisho hayo.
” Tumekuwa na wanafunzi kutoka shule mbalimbali ambao tumewapa elimu kuhusu masuala ya makumbusho ambayo wameyafurahia” alisema Ngereza.
Alisema kumekuwa na changamoto kwa wanannchi kutojua masuala ya makumbusho kama ilivyo kwa nchi zingine duniani.
Alisema ni vizuri sasa kukawa na makongamano, semina na midahalo maeneo mbalimbali ya kufundishana masuala ya makumbusho ambayo ni muhimu kwa nchi yoyote duniani.
“Katika maadhimisho haya kitu kikubwa kilicho nifurahisha ni jinsi wanafunzi walivyo kuwa na kiu ya kuuliza maswali mengi kutaka kujua makumbusho” alisema Ngereza.
Ngereza alisema mwaka huu Tanzania imeungana na nchi zaidi ya 158 duniani kuadhimisha siku hiyo chini ya kauli mbiu isemayo The Future of Museums Recover and Re imagine.
Akizungumzia kuhusu Makumbusho hayo alisema kazi kubwa walioifanya ni kutoa elimu ya kuwajengea uelewa wananchi juu ya kutembelea makumbusho kama sehemu ya kupata elimu na burudani kuhusu urithi wa nchi wa kale na wa Sasa wa Asili Mazingira Utamaduni Sayansi,Teknolojia na Historia.
Dkt. Tungereza alisema tangu asubuhi makumbusho ya jijini Arusha ilikuwa wazi ambapo wananchi wakiwepo wanafunzi walipata fursa ya kuitembelea.