Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na chakula Bi.Josephine Omolo,akifungua semina ya siku mbili kwa waandishi wa habari juu ya uchafuzi wa Sumukuvu na athari zake katika Usalama wa Chakula ,Afya na Uchumi yenye lengo la kuripoti na kutoa elimu juu ya tatizo la sumu kuvu iliyoanza leo Mei 18,2021 jijini Dodoma.
………………………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
Katika kuhakikisha inapanua wigo wa uelewa na kuripoti kwa usahihi kwa jamii juu ya madhara yatokanayo na sumu kuvu Wizara ya Kilimo kupitia mradi wa kudhibiti sumu kuvu TANPAC imeanza kutoa elimu kwa waandishi wa habari namna ya kuripoti na kutoa elimu juu ya tatizo la sumukuvu.
Semina hiyo inalenga kumpa mwandishi uelewa mpana ambaye yeye atakuwa kiungo baina ya Jamii lakini pia Serikali katika kudhibiti na kuzuia tatizo la sumukuvu.
Akizungumza leo Mei 18,2021 jijini Dodoma wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na chakula Josephine Omolo amesema Wizara ya kilimo iliandaa mradi ambao ulizinduliwa mwaka 2019 na kuanza kufanya kazi 2020.
Amesema mradi wa Sumukuvu ulitambuliwa baada ya kugundua madhara kwa wananchi yamekithiri ambapo serikali ikazindua mradi wa kudhibiti uchafuzi wa Sumukuvu katika Usalama wa chakula.
” Tumewapeni Mafunzo nyinyi wanahabari kwasabau nauwezo Mkubwa wa kufikia jamii kwa haraka hivyo mafunzo haya kwenu ni njia mojawapo ya kwenda kuhabarisha jamii juu ya uchafuzi wa Sumukuvu na athari zake kwenye chakula na kuondoa taharuki,” amesema
Ameeleza kuwa Sumukuvu inaleta hofu katika jamii hivyo mkawe mstari wa mbele katika kuwaelimidha jamii juu ya Sumukuvu na tuondoe tahariki katika jamii kwani sumukuvu ilikuwepo yangu hapo zamani,” amesema Omolo
Kwa Upande wake, Mwanaidi Kiya kutoka Wizara ya kilimo Kitengo Cha Usalama na Uhakika wa chakula amesema Takwimu kutoka Shirika la Chakula Duniani (WHO) zinasema kwamba mtu mmoja Kati ya Watu 10 wanakufa kila mwaka kutokana uchafuzi wa chakula.
Ni hapa ambapo amsema kila mwaka Bilioni 110 zinapotea kwenye Kilimo na Takwimu hizo zenaonekana kwenye nchi za kipato Cha chini na zakati kama Tanzania
” Kwa hali hiyo tutashindwa kuendeleza shughuli za Kilimo kwani tumekuwa tukipoteza pesa nyingi,” amesema Kiya.
Nae Mafiti Mkuu Wizara ya kilimo Dkt Analice Kamala amesema Sumukuvu tangia zamani ambapo wengi waliathilika kwa kupata ulemavu wa viungo jambo lilioitwa nalaana.
Vilevile ametaja aina 400 za Sumukuvu zilizovumbuliwa na wataalamu wa afya ambapo chakula kinaweza kuwa na Sumukuvu kama Mkulima hakuzingatia sheria za utaratibu wa Kilimo mwanzo Kilimo mpaka Mwisho wa mavuno.
Hata hivyo amesema Chakula kinaweza kisiwe Salama kipindi Cha mazao yanapokuwa shambani, kipindi Cha mavuno,kipindi Cha mauzo na kipindi Cha udafirishaji kama tu Mkulima hata tumia utaratibu hukika wa Kilimo hautofuatwa.
Madhara ya Sumukuvu yanaweza kujitokeza ndani ya muda mfupi au muda mrefu na itategemea ni kiasi gani Cha chakula kilicholiwa.
Pia amewataja Watu walipo hatarini kuathiriwa na Sumukuvu nipamoja na watoto walio chini ya Mika mitano kupata udumavu ,wagonjwa kutokana na kingazao za mwili kuwa chini,wazee na wamama wajawaziti.
Wizara ya kilimo unatekeleza mradi wa kudhibiti Sumukuvu hapa Nchini kwa lengo la kuimarisha Usalama wa chakula na kuboresha afya ya wananchi katika uelimusha jamii kwa kutumia Vyombo vya habari.
Awali Mratibu wa Mradi wa Sumukuvu Bw.Clepin Mbekomize,amesema kuwa mradi huo umelenga kudhibiti na kutoa elimu juu ya tatizo la Sumukuvu ili iweze kudhibtiwa ipasavyo katika mazao ya chakula.
Bw.Mbekomize amesema kuwa Waandishi wa habari wanapaswa kutumia kalamu zao kwa ajili ya kuondoa taharuki kwa wananchi juu ya suala zima la Sumukuvu katika mazao ya chakula.
“Naiomba jamii isiwe na wasi wasi kuhusiana na Sumukuvu Wizara ya Kilimo pamoja na taasisi zinazohusiana na masuala ya chakula wako mstari wa mbele kukabiliana na changamoto hiyo,”amesema Mbekomize
Hata hivyo Bw.Mbekomize amesema kuwa mara baada ya warsha hii ya siku mbili kwa waandishi wa habari wataenda kutoa elimu kupitia kalamu zenu katika maeneo mbalimbali hapa nchini.