RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na baadhi ya Viongozi alipowasili katika eneo linalotarajiwa kujengwa kwa Bandari ya Kisasa Mwangapwani Wilaya ya Kaskazibi “B” Unguja, akiwa katika ziara yake kutembelea eneo hilo leo 18-5-2021.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Ndg.Makame Machano Haji akitowa maelezo ya eneo la Ujenzi wa Bandari ya Kisasa Mwangapwani Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja wakati wa ziara yake kutembelea eneo hilo na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe.Ayoub Mohammed Mahmoud na (kulia kwa Rais) Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Mhe. Rahma Kassim Ali.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Ndg.Amour Hamil Bakari, akitowa maelezo ya michoro ya Ramani ya eneo la Ujenzi wa Bandari ya Kisasa katika eneo la Mwangapwani Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja wakati wa ziara yake kujionea eneo hilo linalotarajiwa ujenzi huo na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe,Ayoub Mohammed Mahmoud.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kutaka ufafanuzi, kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe.Ayoub Mohammed Mahmoud,wakati wa ziara yake kutembelea eneo linalotarajiwa kujengwa Bandari ya Kisasa katika eneo la Mwangapwani Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja, akiwa katika eneo la Mradi wa Island Petroleum Group.tayari limejengwa matangi ya mafuta.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza CEO wa Kampuni ya United Petroleum Ndg.Collins Chemngorem, akiwa katika ziara yake katika eneo linalotarajiwa ujenzi wa Bandari ya Kisasa Mwangapwani Wilaya ya Kaskazini “B”Unguja, na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe.Ayoub Mohammed Mahmoud na (kulia kwa Rais) Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Mhe.Rahma Kassim Ali.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar.(hawapo pichani) baada ya kumaliza ziara yake kutembelea eneo la Ujenzi wa Bandari ya Kisasa Mwangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja.(Picha na Ikulu)