Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB – Ruth Zaipuna, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza – Salum Kalli, Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa – Baraka Ladislaus (Kulia Mwisho), Afisa Mkuu wa Rasilimali watu wa Benki ya NMB – Emmanuel Akonaay (wa pili kutoka kulia) Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB – Filbert Mponzi (wa pili kushoto) na Mkuu wa Idara ya Kadi wa NMB – Philbert Casmir (Mwenye fulana nyeupe) wakifurahia jambo muda mfupi baada ya uzinduzi rasmi wa mikopo ya boda boda na piki piki za miguu mitatu inayoitwa ‘Mastaboda Loan’ leo jijini Mwanza
Zoezi la kufungua akaunti likiendelea mara baada ya uzinduzi wa Mastaboda Loan.
Sehemu ya waalikwa katika uzinduzi wa Mastaboda Loan.
Mameneja wa NMB matawi ya Mwanza mjini, wakitambulishwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mastaboda Loan
……………………………………………………………………………………….
Benki ya NMB imezindua huduma ya Mikopo ya pikipiki za miguu miwili na miguu mitatu kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa na kuahidi kutumia zaidi ya shilingi Bilioni 5 kutoa mikopo kwa vijana zaidi ya elfu 75 nchini.
Akizungumza katika uzinduzi wa mikopo hiyo kwa vijana waendesha bodaboda na pikipiki za miguu mitatu jijini Mwanza, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna aliwataka wanufaika kujitokeza na kuchagamkia fursa hiyo.
Alisema ikiwa vijana na watu wengine waliojiunga katika umoja wa waendesha bodaboda na pikipiki za miguu wajitokeze na kuchangamkia fursa hiyo, NMB inaweza kuongeza kiwango cha utoaji mikopo kwa baadae.
Ruth alisema kwa mara ya kwanza walizindua huduma hiyo jijini Dar es Salaam mwezi uliopita na sasa ni zamu ya jiji la mwanza huku akisisitiza kuwa wote wamepata elimu ya fedha, ikiwemoo nidhamu ya fedha.
“Hatutaki mikopo hii iwe mizigo kwenu bali baraka kwenu na NMB imedhamiria kufika katika mikoa mingine hapa nchini kwa ajili ya utoaji wa mikopo hii,” alisema Ruth
Nae, Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara Benki ya NMB – Filbert Mponzi alisema uzinduzi wa mpango huo ni pamoja na NMB kuandaa mfumo wa malipo ya Master Boda QR utakaomuwezesha mteja kumlipa bodaboda nauli kiurahisi.
Ili kupata mkopo huu, lazima kila mwanachama wa umoja wa waendesha bodaboda na pikipiki ya miguu mitatu afungue akaunti ya NMB na kuanza kuingiza fedha anayolipwa na wateja kama nauli walau kuanzia miezi mitatu.
Mponzi aliwaomba watanzania kukatia vyombo vyao vya moto Bima kupitia benki ya NMB. Akizindua mpango mikopo huo, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Salum Kalli aliwahakikishia usalama waendesha bodaboda na pikipiki za miguu mitatu muda wote watapokuwa kazini.
Aidha, aliwataka kuheshimu mikopo watakayopatiwa ili iweze kuwasaidia na kusaaidia makundi mengine ya kijamii katika jiji la Mwanza na maeneo mengine.