………………………………………………………………………
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia OSCAR MWASOMI [18] Mfanyabiashara na Mkazi wa Maanga Jijini Mbeya kwa tuhuma za mauaji ya Mwanafunzi wa Chuo cha Biashara Tawi la Mbeya – CBE aitwaye GEOFREY NYONI [20].
Ni kwamba mnamo tarehe 17.05.2021 majira ya saa 23:00 usiku huko Mtaa na Kata ya Sinde, Tarafa ya Sisimba, Jiji na Mkoa wa Mbeya. OSCAR MWASOMI [18] na mtu mmoja aliyefahamika kwa jina moja la MADENGE wakishirikiana na wenzao wanne walimshambulia kwa vitu butu GEOFREY NYONI [20] sehemu mbalimbali za mwili wake na kupelekea kifo chake.
Chanzo cha tukio ni watuhumiwa kumtuhumu marehemu kuiba simu na nguo za MADENGE ambaye ni mpangaji mwenzake katika nyumba waliyopanga. Msako wa kuwatafuta watuhumiwa wengine waliohusika katika tukio hili unaendelea.
WATATU WATIWA MBARONI WAKIWA NA DAWA ZA KULEVYA [HEROINE].
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa watatu 1. VICTOR PATRICK [45] 2. DANIEL NDUNGULU [38] na 3. ALLEN ALFAN [41] wote wakazi wa Kyela kwa tuhuma za kupatikana na dawa za kulevya aina ya Heroine kete 07.
Watuhumiwa walikamatwa katika msako uliofanyika mnamo tarehe 17.05.2021 majira ya saa 15:20 alasiri huko Mtaa wa uwanja wa siasa uliopo Kata ya Mbugani, Tarafa ya Unyakyusa, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya. Watuhumiwa walikamatwa wakiwa ndani ya chumba wakitumia dawa hizo za kulevya. Watuhumiwa watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.
ATIWA MBARONI AKIWA NA MALI YA WIZI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia JUMA MWAILENGE [27] Mkazi wa Igogwe – Kiwira kwa tuhuma za kupatikana na mali ya wizi TV flat screen aina ya Aborder inchi 24.
Mtuhumiwa alikamatwa mnamo tarehe 17.05.2021 majira ya saa 13:46 mchana huko Stendi ya Daladala iliyopo Kata ya Bulyaga, Tarafa ya Tukuyu Mjini, Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya.
Wakati huo huo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa 11 kwa tuhuma za kufanya fujo Stendi za mabasi ya abiria @ Daladala kwa kuyazuia mabasi hayo yasifanye safari zake za kusafirisha abiria maeneo mbalimbali ya Jijini Mbeya baada ya kusitisha mgomo uliodumu kwa takribani wiki moja.