……………………………………………………………………………………….
Na Mwamvua Mwinyi,Bagamoyo
MADIWANI wa halmashauri ya Bagamoyo ,wamedhamiria kulifufua Shirika la maendeleo ya Bagamoyo (BADECO ) ,kuwa sehemu ya mradi mkakati kusaidia kuinua uchumi na kuongeza pato la ndani la halmashauri hiyo .
Eneo hili lilikuwa kitambulisho cha wilaya kwakuwa kivutio ikiwemo watalii lakini kutokana changamoto mbalimbali lilikufa na sasa imebakia magofu na baadhi ya watu wakiendelea kujinufaisha kiholela bila utaratibu,”;Anasema mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo Muhammed Usinga.
Usinga ambae pia ni diwani wa kata ya Yombo akielezea kuhusu walivyojipanga kuibua vyanzo vipya na kufufua maeneo ya kiuchumi ili kujiongezea mapato ,alisema Badeco inapaswa kufufuliwa kwa manufaa ya wilaya.
Alieleza kuwa ,hatua wanayoichukua kwanza ni kutoa matangazo kukaribisha wadau na wawekezaji watakaokaa nao meza moja kuona namna ya kutimiza lengo lao .
“Tunatarajia kuongeza vyanzo vya mapato ya halmashauri na maeneo ya utalii ,”:;hivyo basi Usinga amewaomba wawekezaji wajitokeze kuijenga BADECO mpya kwa kufuata maelekezo ya wataalamu wa halmashauri.
Nae diwani wa kata ya Dunda ,Hafsa Kilingo alisema, BADECO maarufu kama BADECO Beach ilikuwa gumzo nchini ambayo watu wengi walikuwa wakitoka maeneo mbalimbali kwenda kwenye kivutio hicho .
Hafsa alitaka wawe na msimamo wa kweli ,na kuacha kuangalia walipotoka na badala yake wasimamie mipango waliyojiwekea ili kuinua pato la halmashauri na maendeleo ya wilaya.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Zainab Kawawa alisisitiza kuibuliwa kwa vyanzo vipya vya mapato.
Alibainisha kwamba , moja ya vyanzo vinavyopigiwa kelele bila matokeo ni BADECO .
Zainab alisema ,ameshazungumzia sana kuhusu suala hilo ambapo watendaji na madiwani wa halmashauri wanatakiwa kulisimamia na kuchukua hatua kwa maslahi ya wilaya.