Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI (anayeshughulikia elimu) Bw.Gerald Mweli,akizungumza na wajumbe wakati akifungua Mkutano wa 11 wa Umoja wa Makatibu Tawala na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa (TOA) unafanyika kwa siku tatu kuanzia leo Mei 16 hadi 18 jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI (anayeshughulikia elimu) Bw.Gerald Mweli,akisisitiza jambo kwa washiriki wa Mkutano wa 11 wa Umoja wa Makatibu Tawala na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa (TOA) unafanyika kwa siku tatu kuanzia leo Mei 16 hadi 18 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Zainab Chaula,akizungumza na wajumbe wakati wa Mkutano wa 11 wa Umoja wa Makatibu Tawala na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa (TOA) unaofanyika kwa siku tatu kuanzia leo Mei 16 hadi 18 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Zainab Chaula,akionyesha Mwongozo wa Anuani za Makazi na Postikodi kwa wajumbe wakati wa Mkutano wa 11 wa Umoja wa Makatibu Tawala na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa (TOA) unaofanyika kwa siku tatu kuanzia leo Mei 16 hadi 18 jijini Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa TOA, Erick Mapunda,akizungumza wakati wa Mkutano wa 11 wa Umoja wa Makatibu Tawala na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa (TOA) unaofanyika kwa siku tatu kuanzia leo Mei 16 hadi 18 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Clarence Ichwekeleza,akitoa mada ya mfumo wa anuani za makazi na postikodi kwa wajumbe wakati wa Mkutano wa 11 wa Umoja wa Makatibu Tawala na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa (TOA) unaofanyika kwa siku tatu kuanzia leo Mei 16 hadi 18 jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakifatilia hotuba ya Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI (anayeshughulikia elimu) Bw.Gerald Mweli (hayupo pichani) wakati akifungua Mkutano wa 11 wa Umoja wa Makatibu Tawala na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa (TOA) unaofanyika kwa siku tatu ulioanza leo Mei 16 hadi 18 jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI (anayeshughulikia elimu) Bw.Gerald Mweli,akifatilia mada mbalimbali zinazotolewa na washiriki wa Mkutano wa 11 wa Umoja wa Makatibu Tawala na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa (TOA) unaofanyika kwa siku tatu ulioanza leo Mei 16 hadi 18 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Zainab Chaula,akijibu maswali ya wajumbe mara baada ya kuwasilisha Mwongozo wa Anuani za Makazi na Postikodi wakati wa Mkutano wa 11 wa Umoja wa Makatibu Tawala na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa (TOA) unaofanyika kwa siku tatu ulioanza leo Mei 16 hadi 18 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Zainab Chaula,akimkabidhi Mwongozo wa Anuani za Makazi na Postikodi Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI (anayeshughulikia elimu) Bw.Gerald Mweli,wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 11 wa Umoja wa Makatibu Tawala na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa (TOA) unaofanyika kwa siku tatu ulioanza leo Mei 16 hadi 18 jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI (anayeshughulikia elimu) Bw.Gerald Mweli,akimkabidhi Mwongozo wa Anuani za Makazi na Postikodi Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora Msalika Makungu wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 11 wa Umoja wa Makatibu Tawala na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa (TOA) ulioanza leo Mei 16 hadi 18 jijini Dodoma.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora Msalika Makungu akimkabidhi Mwongozo wa Anuani za Makazi na Postikodi Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Bi.Tina Sekambo, wakati wa ufunguzi wa Mkutano 11 wa Umoja wa Makatibu Tawala na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa (TOA) unaofanyika kwa siku tatu ulioanza leo Mei 16 hadi 18 jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI (anayeshughulikia elimu) Bw.Gerald Mweli,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua Mkutano wa 11 Umoja wa Makatibu Tawala na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa (TOA) unaofanyika kwa siku tatu ulioanza leo Mei 16 hadi 18 jijini Dodoma.
……………………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,Gerald Mweli amewataka Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi kuanzisha mtandao kwa ajili ya kujifunza na kubadilishana uzoefu katika utekelezaji wa Miradi ya maendeleo.
Agizo hilo amelitoa leo Mei 16,2021 wakati akifungua Mkutano wa 11 wa Umoja wa Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa (TOA),unaofanyika kwa siku tatu Jijini Dodoma wenye kauli mbiu ya mipango na bajeti inayozingatia huduma endelevu za jamii.
Bw.Mweli amesema kwa sasa kumekuwa na changamoto kubwa ya kusuasua kwa utekelezaji wa miradi katika baadhi ya halmashauri pamoja na Serikali kutoa fedha kwa pamoja na kwa wakati
“Kuna baadhi ya halmashauri zimepelekewa fedha za ujenzi wa mabweni shilingi Mil 80, kuna wengine wamemaliza na kuweka na vitanda lakini wengine bado. Hata pale serikali inapotoa fedha za ujenzi wa madarasa halmashauri mmoja inaweza kuona Sh milioni 20 zilizotolewa hazitoshi lakini kuna wengine kwa kiasi hicho hicho wanamaliza na madawati ndani, sasa kutumia mkianzisha mtandao huo itakuwa rahisi kushirikisha wenzako uzoefu huo ili nao waweze kamilishe mradi huo” amesema Mweli.
Ameendelea kufafanua kuwa uanzishwaji wa mtandao wa kujifunzia kutasaidia kujifunza changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika Halmashauri hasa katika suala zima la utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini.
Aidha Mweli amewataka watendaji hao kutumia mtandao huo kubadilishana uzoefu kuhusu njia mbora ya utekeleza miradi ya maendeleo katika maeneo yao kwa kutumia mfumo wa force akaunti na kwa kutumia mkandarasi.
Amesema kuwa Serikali kwa sasa inaanza kutoa fedha kwa ajili ya halmashauri mpya ambazo hazina makao makuu kwa ajili ya ujenzi wa ofisi, jambo ambalo nataka niwasisitizie ni kwamba hili si jipya Tanzania kuna halmashauri zimejenga ofisi kwa kutumia fedha za ndani hivyo badilishaneni uzoefu wa kati ya halmashauri mmoja na nyingine.
“ Mfano kwenye sekta ya elimu tunamatatizo kwenye ujenzi wa mabweni, kuna halmashauri zimemaliza ujenzi na zingine bado wakati ni maeneo yanafanana, labda kuna sababu basi tutumie mtandao huo kushirikishana maana siku ya mwisho miradi hii ikamilike.”amesisitiza mweli
Hata hivyo Mweli amewataka kusimamia vizuri rasimali watu katika maeneo yao kwa kuzingatia sheria kanuni na taratibu, miongozo na nyaraka zinazosimamia utumishi wa umma
“ Jambo hili limekuwa likituchukulia muda mwingi sana, pale Ofisi ya Rais Tamisemi kwa kusikiliza rufaa kwa baadhi ya watumishi ambao kwa namna moja au nyingine wanaona hajatendewa haki lakini pia tumekuwa tukipata malalamiko mengi kwa watumishi wapya wa kada ya afya pindi wanaporipoti kazini kwa mara ya kwanza kumekuwa na ucheleweshaji sana wa kuwapa fedha za kujikimu.
Awali, Makamu Mwenyekiti wa TOA, Erick Mapunda amesema kuwa kikao hicho kimelenga kujadili njia bora ya kuimarisha utoaji huduma kwa wananchi katika sekta mbalimbali.
, Mapunda amesema kuwa Chama chao kinakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwamo ya wanachama kutolia ada zao jambo ambalo linakifanya chama hicho kuwa tegemezi.
“ Kwa sasa tunadai takribani shilingi milioni 500 kama ada za wanachama ambao wamekuwa hawalipi jambo ambalo litufanya tushindwe kujiendesha na kuwa tegemezi.”amesema Mapunda
Kwa upande wake Mkurugenzi wa idara ya mawasiliano, Clarence Ichwekeleza,akiwasilisha mada ya mfumo wa anuani za makazi na postikodi, amesema kuwa kukamilika kwa program hiyo kutasaidia mamalaka za serikali za mitaa katika kukusanya mapato na kuongeza mapato.
Bi.Clarence amesema kuwa mpaka sasa kata 131 zimefikiwa kati ya kata 3,956 na kuwahimiza watendaji hao kuhakikisha wanarasimisha barabara za mitaa ili kuhakikisha utekelezaji wa mradi huo pindi itakapofika katika maeneo yao.