Sheikh wa Mkoa wa Mwanza, Alhaji Sheikh Hasani Kabeke, akiongoza sala ya Idd iliyofanyika kwenye Uwanja wa Nyamagana jana jijini humu
Waumini wa Dini ya Kiislamu jijini Mwanza wakiswali sala ya Idd kwenye Uwanja wa Nyamagana jana.
Alhaji Sheikh Hasani Kabeke, akisoma dua wakati wa ibada la sala ya Idd jana kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.
Waumini wa Dini ya Kiislamu jijini Mwanza, wakimsikiliza Sheikh wa Mkoa wa Mwanza, Alhaji Sheikh Hasani Kabeke.
**********************
NA BALTAZAR MASHAKA, Mwanza
WAUMINI wa Dini ya Kiislamu ili wafanikiwe na kufikia malengo ya maendeleo wameaswa kuepuka kufarakana, wajenge umoja na kushikamana.
Pia wamekumbushwa kutoa zaka kwa sababu inasafisha mali zao, kuondoa ukame kwenye nchi na watakuwa wanatimiza nguzo ya tatu ya dini ya Kiislamu.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Sheikh wa Mkoa wa Mwanza, Alhaji Sheikh Hasani Kabeke, wakati wa hotuba baada ya sala ya idd iliyofanyika kwenye Uwanja wa Nyamagana, jijini humu.
Alisema waislamu wasipokuwa wamoja na kushikamana katu hawatafanikiwa wala kufikia malengo yao ya maendeleo kwa sababu wakifarakana nguvu yao itapungua.
“Ikifika mahali tukabomoana wenyewe kwa wenyewe sababu ya kuhitlafiana hatuwezi kufanikiwa, ni wajibu wetu kuzika tofauti bila kufarakana bila hivyo ni vigumu kufanikiwa, kila mmoja amheshimu mwinginemaana uislamu ni dini ya amani,inapaswa kuwa kielelezo,”alisema Sheikh Kebeke na kuhoji, kama wanaweza kushirikiana na kukaa na waumini wa dini tofauti iweje wenyewe kwa wenyewe washindwe?
Alisema njia pekee ya kuwavusha kuelekea kwenye maendeleo ni umoja na mshikamano badala ya mifarakano,watu kugombea uimamu misikitini au uenyekiti, ikitokea mtu kaondolewa kwenye uongozi isiwe nongwa.
“Kung’ang’ania uongozi kunasababisha uvunjifu wa amani, hivyo Waislamu tusibali kuleta chokochoko,kuyakubali hayo uislamu utachafuliwa na watu wachache kwa maslahi yao,”alisema Sheikh Kabeke.
Aidha aliwaasa waumini hao wasiiche miskiti tupu bali waudumu katika mema na kuyaishi yote ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kutoa zaka kwa sababu Mtume Muhhamad S.A.W. anasema siku ya kiyama fedha yako itageuga shaba na itakuchoma hivyo kila mmoja wajibike kulipa zaka kwa mujibu wa sheria ya dini.
Sheikh huyo wa Mkoa wa Mwanza, alisema kuwa nyeabudiwa ni Mungu mmoja na si wawili, hivyo waislamu wasijione funga yao am kushinda njaa kwao kwa ibada hiyo si jambo geni bali watafaradhishwa kabl sababu lengo na dhamira ya saum hiyo ni kumcha Mungu.
Hata hivyo, alionya wale ambao walishindwa kufunga Ramadhani wakisingizia maradhi wataingia motoni na kuwashukuru waliojaaliwa kuwa miongoni mwa waliotwa kwa jina tukufu.