MKURUGENZI wa Idara Huduma za Rais Ikulu Zanzibar (Mnikulu) Ndg. Mahmood Hashim Othman, akizungumza na kuwasilisha salamu za Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi, kwa Wazee wa makundi maalum waliofika Ikulu kwa ajili ya kukabidhiwa Sikukuu iliotolewa na Rais, hafla hiyo imefanyika katika Ofisi ya Mnikulu Ikulu Jijini Zanzibar.
MKURUGENZI Idara Huduma za Rais Ikulu Zanzibar (Mnikulu).Ndg. Mahmood Hashim Othman , akimkabidhi mmoja wa Wazee wa Makundi Maalum Bw. Subira Haji Mlenge, mchele na fedha, akikabidhi kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, kwa ajili ya kusherehekea Sikukuu ya Eid El Fitry,hafla hiyo imefanyika katika Ofisi ya Mnikulu Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)