Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini wa kati kati Silvestry Koka akiwa katika picha ya pamoja na wahanga ambao nyumba zao mbili zilizopo katika mtaa wa Muharakani na Mkuza katika zilizopo Wilaya ya Kibaha zimeungua kwa moto na kusababisha hasara kubwa ikiwemo kuteketea kwa mali zote za ndani
Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka wa kulia akiwa anamfariji mmoja wa mtoto mdogo akiwa abebemwa na mama yake baada ya kunususirika kupoteza miasha baada ya nyumba yao waliyokuwa wakiishi kuungua kwa moto na kuteketeza mali zote za ndani.
Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka akiwa ameambatana na baadhi ya viongozi wa Chama cha mapinduzi (CCM) wakiangalia nyumba ambayo iliungua kwa moto na kuteketeza vifaa na mali zote.
kushoto ni mmoja wa wahanga wa tukio la janga la moto akikabidhiwa msaada wa fedha kutoka kwa Mbunge wa jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka ambaye alifunga safari kwa ajilli ya kwenda kuzitembelea familia ambazo zimepatwa na majanga hayo.
Mwenyekiti wa mtaa wa Muharakati uliopo kata ya picha ya ndege Eliamini Mgonja akitoa ufafanua juu ya tukio hilo kwa Mbunge wa jimbo la Kibaha mjini hayupo pichani ambaye alikwenda kwa ajili ya kuwafariji na kutoa msaada wa fedha.
Katibu wa UWT katika halmashauri ya Kibaha mji kushoto Elina Mngoja akimpa maelekezo Mbuge mara baada ya kwenda kuzipa pole familia ambazo zimekumbwa na janga la kuunguliwa na nyumba zao mbili.
Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini wa kati kati aliyenyoosha mkono akitoa maelekezo kwa baadhi ya viongozi wa chama ambao waliambatana naye katika kwenda kuona athari amabzo zilijitokeza baada ya nyumba hizo kuungua na moto.(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU)
……………………………………………………………………………………………….
NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
KAYA zipatazo sita zimenusurika kupoteza maisha yao katika eneo la mitaa miwili ya Muharakani na Mkuza Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani baada ya nyumba zao walizokuwa wakiishi kupata janga la kuunguliwa na moto na kusababisha uharibifu mkubwa ambao umepelekea kuteketea kwa mali zao zote huku wakiwa katika hali ya sintofahamu kutokana na kukosa makazi ya kuishi.
Kufuatia tukio hilo Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini kupitia tiketi ya Chama cha mapinduzi (CCM) Silvestry Koka ametembelea katika eneo la tukio akiwa ameambatana na baadhi ya vongozi wa serikali pamoja na viongozi wa Chama na kujionea uharibufu ambao umejitokeza ambapo amewafariji wahanga waliounguliwa na nyumba zao kwa kuchangia kiasi cha shilingi milioni 1.2 ambazo zitaweza kuwasaidia kujikimu katika kipindi hiki kigumu walichonacho.
Koka alibainishwa kwamba amesikitishwa sana na tukio hilo la moto ambalo limeweza kuwafanya baadhi ya wananchi ambao walikuwa wanaishi katika nyumba hizo kuishi katika mazingira ambayo sio rafiki ndio maana akaamua kuacha mambo mengine kwa ajili ya kwenda kuwafariji wahanga hao ambao kwa kweli mali zao zote zimetekea kwa moto na mimi nitaendelea kuwapa sapoti kadiri ya uwezo wangu.
“Mimi kama Mbunge wenu wa Jimbo la Kibaha mjini tukio hilo la wananchi wangu kupatwa na janga la moto limenishitua sana na kwamba nilipatiwa taarifa hizi wakati nipo katika vikao mbali mbali vya Bunge lakini kutokan na hali jinsi ilivyo na wananchi wamepoteza mali zo na kuunguliwa na vitu mbali mbali imelazimu sasa niache shughuli zingine ili nije nije kuangalia hali halisi ya tukioa na nimeweza kuona hivyo nimechangia kiasi cha shilingi milioni 1.2 na huu ni mwanzo tuu,’alisema Koka.
Aidha Mbunge huyo alisema kwamba licha ya kwamba familia hizo zipo katika wakati mgumu wa kupata janga la kuunguliwa na nyumba zao ataendelea kushirikian nao bega kwa bega katika kipindi chote cha tatizo hili kwani pamoja na kutoa fedha hizo lakini bado kuna michango mingine ambayo inahitajika ili wananchi hao waweze kurejea katika hali yao ya kawaida.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa wa Mtaa wa Muharakani alibainisha kwamba majirani waliweza kufanya jihihada zote kwa ajili ya kuuzima moto huo ili kuokoa mali zilizokuwa ndali lakini walishindwa kufanikiwa na kusababisha mali zote kuteketea na moto huku akibainisha hakuna mtu yoyote aliyepoteza maisha kwani waliwahi kutoka nje.
“Mheshimiwa Mbunge kwanza sisi kama wananchi wako tumefarijika sana kwa ujio wako maana kwa kweli hizi kaya kwa sasa zipo katika mazingira magumu lakini msaada wako huu utaweza kusaidia kununua mahitaji mbali mbali amabyo ni muhimu maana siku ya tukio tulijitahidi kupambana kuokoa mali lakini tulishindwa kabisa na gari la zima moto pindi lilipofika tayari vitu vyote vilikuwa vimeteketea,”alibainisha Mwenyekiti.
Nao baadhi ya wahanga wa janga hilo la moto hawakusita kumpongeza Mbunge huyo wa Jimbo la Kibaha mjini kwa kuamua kuacha vikao vinavyoendelea Bungeni na kwenda kuwafariji pamoja na kuwapatia msaada wa fedha ambazo zitaweza kuwasaidia katika baadhi y mahitaji muhimu na kuiomba serikali na wadau wengine kuwasaidia msaada wa hali na mali ili waweze kijikimu kimaisha.
“Kwanza kabisa tunapenda kutoa shukrani zetu za kipekee kwa baba yetu ambaye ni Mbunge wetu wa Jimbo la Kibaha mjini Koka kwani ni viongozi wachache sana ambao wana moyo kama wake kwani ameweza kuacha shughuli zake mbali mbali ikiwmeo vikao vya Bunge ili kuweza kuja kutufariji na kutupa msaada huu hivyo tunamshukuru sana Mbunge wetu”alisema wahanga hao.
Pia aliongeza kuwa pamoja na kupatiwa msaada huo lakini kutokana na ukubwa wa tukio hilo wamesema kwamba bado wahahitaji msaasa wa vitu mbali mbali ikiwemo nguo, vyakula, pamoja na mahitaji mengine na kuimba serikali kuiliangalia zaidi jambo hili kwa jicho la tatu kwa lengo la kuwasaidia katika jambo hilo ambalo limewafanya waweze kurudi nyuma katika kutimiza malengo yao.
Tukio hilo la janga la moto limetokea hivi karibuni katika mtaa wa Muhazakani pamoja na mtaa wa mkuza Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani na kusababisha nyumba mbili kuungua na kaya sita kukosa makazi ya kuishi kutokana na mali zote zilizokuwemo ndani kuteketea kwa moto na kwamba inadaiwa chanzo cha moto huo ni itirafu ya umeme.