*********************
Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam imewataka wafanyabiashara waliojenga vibanda katikati ya Jiji la Dar es Salaam kuviondoa ikiwani kutekeleza sheria ya mipango miji.
Hayo yamejiri leo jijini Dar es salaam katika kikao cha baraza la madiwani wa jiji La Dar es salaam ambalo limeongozwa na Mwenyekiti wa Baraza hilo ambaye ni Mstahiki Meya wa Jiji Omary Kumbilamoto.
Akizungumza katika kikao hicho Afisa uhusiano wa jiji la Dar es Salaam Tabu Shaibu ametolea ufafanuzi suala la wafanyabiashara ambapo amesema hawajazuia wafanyabiashara kuendelea na shughuli zao,bali wanachotakiwa kufanya ni kutojenga vibanda na kuwataka wauze bidhaa zao kwenye meza ili wakimaliza iwe rahisi kuziondoa na kuacha maeneo wazi.
Aidha Afisa Uhusiano huyo amesema mji ni lazima upangike kwa kila eneo linatakiwa kuwa na matumizi sahihi kwani sheria ya mipango miji hairuhusu kujenga vibanda,hivyo amewataka wafanyabiashara hao kutii agizo hilo.
Wakatihuohuo ,Baraza hilo la madiwani wa jiji limepitisha taarifa ya utendaji kazi wa jiji la Dar es Salaam kutoka mwezi Januari hadi Machi 2021ambapo jambo kubwa lililojadiliwa ni pamoja na changamoto kubwa ya miundombinu katika jiji hilo.
Hata hivyo imeelezwa kuwa katika kipindi cha Julai hadi Mei mwaka huu Halmashauriya Jiji la Dar es salaam imekusanya zaidi ya shilingi bilioni 47 sawa na asilimia 78 ya malengo na hivyo jambo lililopelekea kuvuka lengo kwa aslimia 5%.