Mkurugenzi mtendaji wa TAHA Dkt Jackline Mkindi akieleza fursa zilizpo katika zao la Parachichi katika uzinduzi wa kongani la zao hilo kand ya Kaskazini iliyofanyika katika kijiji cha Gyani kata ya Nkoaranga halmashauri ya Meru.
Msaidizi wa katibu tawala mkoa wa Arusha Agney Chitukuro akiongea na wananchi wa kijiji cha Gyani kata ya Nkoaranga katika uzinduzi wa kongani la Parachichi uliofanya ya asasi ya kilele ya sekta binafsi inayojishulilisha na kilimo cha horticuiture[TAHA].
Mkurugenzi mtendaji wa TAHA akipanda mche wa Parachichi katika uzinduzi wa kongani la zao hilo kanda ya Kaskazini lililofanyika halmashauri ya Meru .
Baadhi ya miche ya kisasa ya Parachichi inayotarajiwa kupandwa katika hekari 250 katika kijiji cha Gyani kata ya Nkoaranga halmashauri ya Meru.
***********************************
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Asasi ya kilele ya sekta binafsi inayojihususha na kuendeleza tasnia ya horticulture nchini [TAHA] imezindua kongani la zao la Parachichi kanda ya Kaskazini katika kijiji cha Gyani kilichopo kata ya Nkoaranga halmashauri ya Meru mkoani Arusha kwa kuhamasisha uwekezaji katika zao hilo kutokana na fursa kubwa masoko iliyopo katika soko la kimatifa.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa kongani hilo mkurugenzi mtendaji wa asasi hiyo Dkt Jackline Mkindi alisema kuwa kwa mwaka uliopita uzalishaji wa zao hilo ulikuwa ni tani 39,000 huku uuzaji nje ya nchi ukiwa ni tani 8500 hadi 9000 ambayo iliingiza dola za kimarekani milioni 30 ambapo kwa miaka mitatu ijayo kutokana na uwekezaji zao hilo wanatarajiwa kuingiza zaidi ya bilioni 22 kutokana na uhitaji mkubwa uliopo katika soko la kimataifa.
Dkt Mkindi alisema kuwa wanahamasisha wanchi wawekeze zaidi katika kilimo hicho kwani wana ardhi nzuri, hali ya hewa pamoja na maji ambapo katika kongani hilo mpakasasa limewaunganisha wakulima 200 ambao wameshaandaa eneo la kulima zao hilo hekari 250 pamoja na kununu miche 500 na asasi hiyo kuwapatia miche 500.
“Katika zao hili la Parachichi uzalishaji katika shamba lenye ukubwa wa hekari moja ni tani 2.7 hadi tani 7 ambapo faida yake kama mtu atauza katika soko la kimataifa atapata shilingi milioni 4 hadi milioni 4.5 lakini pia zao hili linaongeza uzalishaji kadri mti unapoongeza miaka na kuzalisha tani 8 hadi kumi ambayo faida yake ni milioni 13 na kama mtu ana hekari nyingi zaidi atapata zaidi,”Alisema Dkt Jackline.
Alifafanua kuwa katika shamba la hekari moja inaweza kuoteshwa miti 120 na gharama ya kuwekeza ni shilingi milioni 1.1 huku gharama ya kuhudumia shamba ikiwa sio zaidi ya shilingi laki tano ambapo TAHA wanaendelea kuwajengea uwezo wakulima juu ya zao hilo pamoja na kuhakikisha kuwa wanazalisha mazao yenye ubora unaohitajika katika soko la kimataifa.
Aidha aliendelea kusema kuwa serikali imewaongezea ufanisi mkubwa wa kuyafikia masoko kwa kuboresha miundombinu ya usafiri ambapo wanasafirisha mazao kwa kupitia nji ya anga na maji na hadi hivi sasa wanauwezo wa kupeleka mazao hayo katika nchi 198 duniani.
Alieleza kuwa zao hilo linafursa nyingi ikiwemo kutunza mazingira, ni tunda, linakamuliwa mafuta pamoja na kokwa lake kutengenezewa bidhaa za kutunza ngozi hivyo ifike mahali wakulima wawekeze katika zao hilo ka wingi kwani linachangia katika ukuaji wa uchumi.
Kwa upande wake msaidizi wa katibu tawala mkoa wa Arusha Agney Chitukuro akimwakilisha kaimu katibu tawala David Lymongi alisema kuwa kama serikali wanafahamu kazi nzuri wanayoifanya TAHA ambapo mkoa kupitia halmashauri zake watashirikiana nao pamoja na kuhakikisha uwekezaji wa zao hilo unafanikiwa kwa asilimia kubwa.
Alisema tasnia ya horticulture imetoa ajira kwa akina mama wengi na vijana na ni fahari ya serikali kuoa kuwa pato la parachichi linapanda kila mwaka ambapo aliwataka wanachi kuchangamkia fursa hiyo kwani ipo na tayari wana uhakika wa masoko.
“ Ni vizuri mnunuzi anapokuja anapata mzigo wa kutosha katika eneo moja hivyo tumieni fursa hii kwani ni uwekezaji wenye faida kubwa na ni wa muda mrefu takriban miaka 40 na nyie Taha nihakikishie kuwa uongozi wamkoa utato ushirikiano wa kutosha ili wakulima waweze kupata faida na kuinua uchumi wao,” Alisema Chitukuro
Diwani wa kata ya Nkoaranga Esau Sikawa aliishukuru TAHA kwa kwa kuwapelekea fursa hiyo na wanaamini kuwa uchumi wao utaenda kuimarika kwani awali walikuwa wanategemea zao la Kahawa ambalo kwa sasa wameshindwa kuendelea nayo kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo kushuka kwa uzalishaji.
Nao baadhi ya wanakikundi wa kongani hiyo akiwemo Moses Kitosio walisema kuwa baada ya Taha kuwaeleza juu ya fursa zilizopo katika zao la Parachichi wamechukua sehemu kubwa kubadili mazao waliyokuwa wakilima ambayo pia waliyarithi kutoka kwa wazazi wao kwani wapokea kwa nguvu kubwa na wanatarajia kunufaika kwa asilimia 100.
Esta Mungure alieleza kuwa wamekuwa na miti yaparachichi ya kienyeji kwa kiasi kidogo lakini pia haikuwa kwaajili ya biashara hivi sasa wanaingia katika kilimo biashara ya zao hilo kwa kupanda miche ya kisasa waliyoletewa ambayo uzalishaji wake ni mkubwa na utawainua kiuchumi hasa wanawake.