********************
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Naibu waziri wa wizara ya katiba na sheria Geoffrey Mizengo Pinda amewataka wananchi na viongozi wote kutambia kuwa takwimu sahihi za vizazi ni kichocheo kikubwa cha uchumi katika nchi kwani itasaidia serikali kupanga mipango yake ya maendeleo kwa usahihi.
Pinda aliyasema hayo wakati akizindua mpango wa usajili wa watoto wa umri chini ya miaka mitano kwa mikoa ya Arusha na Manyara ambapo alieleza halo haikuwa nzuri kwani katika sensa ya mwaka 2012 asilimia 13.4 tuu ya watanzania ndio waliokuwa wamesajiliwa na kupata vyeti vya kuzaliwa.
Adha alitoa wito kwa mikoa yote nchini ambayo imeshafikiwa na zoezi hilo kuhakikisha wanaendelea kusajili kwani kila siku watoto wanazaliwa ikiwa ni pamoja na kuutaka mkoa wa Arusha na Manyara kuingia katika ushindani wa zoezi hilo na itakapofika wakati wa tathimini kila mmoja awe ametoa alipo na kuwa juu.
“Baada ya muda tunataka watu wajekujifunza kwenu watoto hawa zaidi ya laki 6 wawe wamesajiliwa na kuweza kufikisha lengo la kusajili watotozaifi ya milioni 6 kwa nchi
nzima,” Alisema Pinda.
Kwa upabde Emmy Hadson kaimu mkurugenzi mkuu wa RITA alisema kuwa mpango huo umeshaanza kutekelezwa katika mikoa 18 ambapo kwa uzinduzi huo wa mikoa ya Arusha na Manyara watawezakufikisha mikoa 20 na katika mikoa ya mwanzo imeonyesha mafaniko makubwa.
“Lengo la mpango huu ni kuhakikisha watoto wanasajiliwa na kupata haki yao yamsingi ya kupata vyeti vya kuzaliwa ambapo pia tutaenda na katika mikoa mingine iliyobaki,” Alisema Emmy.
Naye mwenyekiti wa bodi ya RITA Prof Hamis Bihenga alisema kuwa wapo katika mikakati wa kuhakikisha kuwa matukio tote muhimu ya binadamu ikiwemo kuzaliwa yanasajiliwa kwani kwa kufanya usajili huo serikali itajua idadi ya watoto wote waliozaliwa na baada ya miaka saba wanahitaji kwenda shule hivyo itasaidia kuondoa changamoto mbalimbali ikiwemo ya madarasa na madawati.
Alisema kuwa zoezi hilo kwasasa linafanyika katika ofisi za kata na katika maeneo yote panapotolewa huduma ya mama na mtoto ili kuondoa mrundikano wa watu wasio kuwa na vyeti vya kuzaliwa hapo baade ambapo usajili kwa sasa asilimia 13.4 na wanatarajia kufikia asilimia 55 huku lengo likiwa kufikia asilimia 100.
“Kazi hii itafanyika kwa awamu mbili ambayo ya kwanza hii lakini pia tutasimika mfumo huu ili uwe endelevu na kama tunavyoona kwa mkoa wa Arusha usajili mpaka sasa ni asilimia 23.2 na mkoa wa Manyara ni asilimia 10.6 hivyo wanajamii wakasajili watoto ILI baade kuseiwe na watoto wanaokuwakutokuwa na vyeti,”Alisema Profesa Bihenga.
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro akimwakilisha mkuu wa wa mkoa Arusha Iddy Kimanta alisema kuwa wananchi wengi mpaka sasa hawajasajiliwa na ndio maana takwimu kwa mkoa wa Arusha zipo chini lakini kwa kuanza kwa utekelezaji huo na kuweza kupata takwimu sahihi hivyo wilaya na halmashauri zote zihakikishe zoezi hilo linafanikiwa kwaasilimi 100.
Alisema kuwa Arusha wameuelewa mpango huo na wamepokea hivyo watahakikisha unafanikiwa katika wilaya zote 6na halmashauri 7 ambapo kata zote 946 zitafanya kazi kwa ufanisi na kuweza kusajiliwatoto zaidi ya laki 3.
Mkoa wa Manyara Joseph Mkirikiti alisema kuwa changamoto kubwa iliyopelekea mkoa wake kuwa chini katika usajili ni pamoja na ukubwa wa mkoa huo kwani kutoka kata moja kwenda kata nyingine ni sawa na kutembea wilaya nzima ya mikoa mingine ambapo pamoja na changamoto hiyo watahakikisha kuwa zoezi hilo linafanikiwa.
“Tumejielekeza kuungua mkono zoezi hili kwani linasaidia kupunguza gharama za upatikanaji wa vyeti wa awali kwani hii ya sasa inawapunguzia wananchi atha ya kupeleka taarifa za awali umbali mrefu na baada ya siku kadhaa kwenda kufuata cheti,” Alisema Mkirikiti.