Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu (hawapo pichani) kuhusu huduma za mawasiliano na intaneti Bungeni, Dodoma. Aliyeketi katikati ni Dkt. Zainab Chaula, Katibu Mkuu na anayesikiliza ni Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Jim Yonazi wa Wizara hiyo
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile akitoa taarifa kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuhusu huduma za mawasiliano na intaneti Bungeni, Dodoma. Aliyeketi wa pili kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Zainab Chaula na wa kwanza kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Anne Kilango Malecela
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Seleman Kakoso akizungumza baada ya Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile (aliyeketi mbele katikati) kuwasilisha taarifa kuhusu mawasiliano na intaneti kwa Kamati hiyo Bungeni, Dodoma. Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Zainab Chaula, akimsikiliza
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Anne Kilango Malecela akichangia mada baada ya Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile (hayupo pichani) kuwasilisha taarifa kwa Kamati hiyo kuhusu mawasiliano na intaneti Bungeni, Dodoma.
Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu akichangia hoja kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu baada ya Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile (hayupo pichani) kuwasilisha taarifa kuhusu mawasiliano na intaneti kwa Kamati hiyo Bungeni, Dodoma
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile (wa kwanza kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Zainab Chaula (wa kwanza kushoto) wakisikiliza kwa makini maoni ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu baada ya kuwasilisha taarifa ya mawasiliano na intaneti kwa Kamati hiyo Bungeni, Dodoma
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Dkt. Jabir Bakari akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu baada ya Waziri wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile (hayupo pichani) kuwasilisha taarifa kuhusu mawasiliano na intaneti kwa Kamati hiyo Bungeni, Dodoma. Wa kwanza kulia ni Katibu wa Wizara hiyo, Dkt. Zainab Chaula na katikati ni Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Jim Yonazi