Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Dkt. Leonard Chamuriho akizungumza na watumishi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) hawapo pichani wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Wakala huo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mjini Dodoma leo.
Baadhi ya watumishi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Dkt. Leonard Chamuriho alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Wakala huo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mjini Dodoma leo.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle akizungumza na watumishi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) hawapo pichani wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Wakala huo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mjini Dodoma leo. Kushoto ni Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Dkt. Leonard Chamuriho na kulia ni Almasi Mzee, Mwenyekiti wa TUGHE TEMESA.
Menejimenti ya Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) katika picha ya Pamoja na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Dkt. Leonard Chamuriho katikati.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Dkt. Leonard Chamuriho kushoto na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle kulia wakipiga makofi wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Wakala huo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mjini Dodoma leo.
Mkurugenzi wa Matengenezo na Huduma za Ufundi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Heriel Mteri akizungumza na watumishi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) hawapo pichani wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Wakala huo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mjini Dodoma leo, kulia ni Almasi Mzee, Mwenyekiti wa TUGHE TEMESA.
*****************************
Na. ALFRED MGWENO TEMESA DODOMA
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Dkt. Leonard Chamuriho ametoa wito kwa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kuongeza idadi ya karakana za wilaya katika maeneo mbalimbali hapa nchini ili kusogeza zaidi huduma hiyo kwa maeneo ambayo yako mbali na karakana za Mikoa na Wilaya.
Dkt. Chamuriho ameyasema hayo leo wakati akizungumza katika mkutano wa Baraza la wafanyakazi la Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Makao makuu mjini Dodoma, amesema mkutano huo ni mahususi na muhimu kwani una lengo la kuboresha utendaji kazi na kushirikisha watumishi kwenye maamuzi ili kufikia lengo la kuongeza ufanisi na tija kwa Wakala.
Aliupongeza Wakala kwa kuanzisha karakana mpya za Wilaya ikiwemo ya Songwe, Same, Ifakara na Kahama kwa lengo la kusogeza huduma karibu pamoja na kukarabati karakana za Mbeya, Mwanza, Vingunguti, Dodoma na karakana ya Mkoa Simiyu ambayo ujenzi wake unaendelea na utakamilika hivi karibuni.
‘’Ninaamini kwamba kuanzishwa kwake kutasaidia mahitaji kwa huduma hiyo kuipata kwa ubora na kwa muda unaohitajika’’ Alisema Dkt. Chamuriho na kuongeza kuwa miundombinu iliyopo TEMESA ndiyo miundombinu mikubwa kuliko miundombinu ya karakana zote hapa nchini.
‘’Mmenunua vifaa stahiki vya karakana zote kwahiyo sasa mmekamilika hivyo ni mategemeo yangu kwamba vifaa hivyo vitatumika kama ilivyokusudiwa na makusudi ni kutoa huduma ambazo zinatarajiwa,’’ alisema Dkt. Chamuriho ambapo aliupongeza pia Wakala kwa kununua ‘Mobile workshops’ mpya sita karakana zinazotembea kwa ajili ya kutoa huduma katika maeneo yaliyo mbali na karakana za mikoa pamoja na mashine za kisasa za mikoa thelathini za kupimia magari ‘diagnosis machine’.
Awali akizungumza katika baraza hilo Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle amesema baraza la wafanyakazi ni muhimu kwani ni chombo au daraja muhimu la ushauri na majadiliano sehemu ya kazi linalosaidia pande zote mbili za mwajiri na mwajiriwa kuboresha mazingira ya kazi za taasisi na kuleta ufanisi na tija.
‘’Wakala hadi sasa una watumishi 527 wa ajira ya kudumu na watumishi 485 wa mkataba, kati ya hao wahandisi ni 92 na mafundi sanifu ni 221’’. Ameongeza Mhandisi Maselle ambapo amesisitiza kuwa Serikali imekwishatoa vibali vya ajira mpya 95 kwa ajili ya mafundi sanifu ambavyo vitatekelezwa katika mwaka huu wa fedha.
Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) una upungufu wa watumishi wa kada ya ufundi 152 ikijumuisha wahandisi 50 na fundi sanifu 102 na kwa mujibu wa Mtendaji Mkuu utaendelea kuajiri watumishi wa mkataba ili kupunguza uhaba wa watumishi kwa kadiri hali ya kifedha itakavyoruhusu.