Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) akisalimiana na Balozi wa Denmark hapa nchini, Mhe. Mette Norgaard Dissing Spandet katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Denmark hapa nchini, Mhe. Mette Norgaard Dissing Spandet akimuelezea jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) wakati walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Balozi wa Urusi nchini, Mhe. Yuri Popov akimsikiliza akimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula wakati balozi huyo alipomtembelea Mhe. Waziri ofisini kwake Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) akipokea zawadi ya picha kutoka kwa Balozi wa Urusi nchini, Mhe. Yuri Popov
**********************************
Na Mwandishi Wetu, Dar
Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika Mhe. James Duddrige anatarajiwa kuwasili nchini Mei 11, 2021 kwa ziara ya siku mbili yenye lengo la kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania na Uingereza ambapo pamoja na mambo mengie, anatarajiwa kukutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na baadae Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akizungumzia juu ya ujio wa Waziri huyo wa Uingereza Mhe. James Duddridge amesema Uingereza ni miongoni mwa nchi zinazoongoza kuwekeza katika sekta ya uwekezaji na biashara hapa nchini hivyo ujio wake ni fursa ya kuangalia maeneo muhimu ya kushirikiana na kufanya biashara miongoni mwa Tanzania na Uingereza.
“Uingereza ni miongoni mwa nchi zinazoongoza kuwekeza katika sekta ya uwekezaji na biashara hapa nchini hivyo ujio wake ni fursa ya kuangalia maeneo muhimu ya kushirikiana na kufanya biashara miongoni mwa Tanzania na Uingereza,” Amesema Balozi Mulamula
Katika tukio jingine Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Shirikisho la Urusi hapa nchini Mhe. Yuri Popov na kujadilia masuala mbalimbali ya ushirikiano ambapo Balozi Mulamula amemsisitizia Mhe. Yuri kuwa wakati umefika sasa kwa Urusi kuongeza uwekezaji hapa nchini katika sekta mbalimbali badala ya kufanya biashara pekee.
Mbali na Balozi huyo wa Shrikisho la Urusi pia Waziri Mulamula amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Denmark Mhe Mette Norgaard Dissing Spandet ambapo ambaye amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyotekeleza majukumu yake na kuongeza kuwa Denmark itaendelea kushirikiana na Tanzania katika masuala ya kidiplomasia,uchumi,uwekezaji na biashara pamoja na suala la mapambano dhidi ya COVID 19 ili kuhakikisha hakuna nchi inayoachwa nyuma kimaendeleo pale dunia iatakapofunguka.