Home Mchanganyiko BARABARA KATA YA SEKEI KUANZA KUTENGENEZWA BAADA YA MVUA ZA MASIKA ZINAZOENDELEA...

BARABARA KATA YA SEKEI KUANZA KUTENGENEZWA BAADA YA MVUA ZA MASIKA ZINAZOENDELEA KUNYESHA KUISHA.

0
*******************************
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Diwani wa kata ya Sekei Gerald John Sebastian kwa kushirikiana na mhandisi wa jiji la Arusha Mhandisi Samwel Mshuza wametembelea barabara korofi katika kata ya sekei mtaa wa Naurei na Sanawari na kuahidi kuwa barabara hizo zitafanyiwa matengenezo baada ya mvua za masika zinazoendelea kunyesha kuisha.
Barabara hizo zilizoharibika vibaya kwasababu ya mafuriko yaliyosababishwa na ukosefu wa mitaro ya kupitishia maji na kusababisha watu kushindwa kufikia huduma za kijamii ikiwemo hosipitali shule na wengine kushindwa kwenda katika shughuli zao za kujiingizia kipato wakati wa mvua kutokana na maji mengi kupita pamoja na kuingia ndani ya  nyumba zao.
Diwani Sebastian alisema kuwa wananchi wa maeneo hayo wamekuwa wakieleza changamoto ya barabara hizo kwa muda mre hali iliyomlazimu kufikisha kero hizo katika uongozi wa jiji na ndipo fedha za dharura zilipotolewa kwaaji ya kutengeneza barabara hizo
“Kutokana na changamoto hii hasa hii ya maji kuingia katika nyumba zaidi ya 50 katika mtaa huu wa Naurei naona fedha zilizotolewa kwaajili ya kurekebisha barabara hii ni muujiza na ni washukuru viongozi wangu akiwemo Mkurugenzi na Meya kwa kuona kuwa kata hii inauhitaji zaidi na kuipa kipaumbele kwani wananchi wanateseka,”Alisema Sebastian.
Alifafanua kuwa ujenzi  unaanza wakati wowote mvua zitakapoisha kwasababu hawawezi kufanya kazi ya hiyo wakati wa mvua hivyo wananchi wawe na matumaini hayo lakini pia watakapotengenezewa hata kama ni kidogo wasibeze bali washukuru kwani utekelezaji mkubwa zaidi utakuja.
”Kwasasa tutaenda kufanya kile ambacho inawezekana ili kupunguza atha hii, muweze kufikia huduma za kijamii pamoja na kuendelea na shughul zenu za kila siku kutokana na fedha iliyopatikana na niwafahamishe tuu fedha hiyo haikuwa kwenye mpango ila ni fedha ya dharura baada ya kukuona kuwa hali ni mbaya,”Aliendelea kusema.
Aidha baadhi ya wananchi akiwemo Lukas Elihau Mollel alisema kuwa changamoto hiyo inasababishwa na watu kuziba njia za maji katika eneo la juu ambapo ili kumaliza kabisa kero hiyo wataalamu hao wanapaswa kutafuta chanzo hicho pamoja na kushirikiana na wananchi kwani wapo tayari kushirikiana nao.
“Maendeleo ni barabara watu wa eneo hili hawawezi kupata maendeleo kama barabara kila mwaka itakuwa hivi hivyo tunaomba mtusaidie kero hii iweze kuisha kabisa wananchi wawe huru katika kazi zao kwani watakuwa na amani ya kutoka na kurudi samala bila jambo lolote kuharibika lakini sasa hivi wakiona tuu dalili ya mvua hata kazi wanashindwa kufanya kutokana na mdhara haya,”Alisema Lukas.
Tabea Lebayo Laizer ambaye pia ni mkazi wa eneo hilo alisema kuwa kwa sasa huduma zinashindikana katika eneo hilo kutokana na magari kushindwa kupita hata akitokea mgonjwana na changamoto hii ni ya muda mrefu na mafuriko hayo pia yanaharibu na miundombinu ya ya maji safi hivyo tunaomba serikali yetu ituangalie itufanya tuifurahie hata kupitia hili.
“Kwa mfano juzi tuu mama mmoja mwenye umri kama wakwangua aliugua ghafla kilichofanyika ni kumbeba hadi eneo la barabara kubwa ya Arusha-Moshi akapakizwa gari na kukimbizwa hosipitali mtaona kuwa hali hii pia inaweza kusababisha vifo kutokana na watu kushindwa kuzifikia hudma za afya kwa haraka,” Alisema Tabea.
Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa huu Nehemia Naing’ola Mollel alisema kuwa kila mwaka maji yanaleta madhara hayo hayo hivyo kama watatengeneza barabara bila kuweka mitaro itakuwa ni kazi bure kwana na mwaka ujao maji hayo yatarudi hivyo wamemuomba mhandisi hiyo kuangalia namna bora ya kuondoa changamoto hiyo kabisa.