Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Mwanaidi Ali Khamis akizungumza katika Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii lililofanyika katika Makao ya Taifa ya Watoto Kikombo Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya-Idara ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akieleza lengo la Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Afya- Iadra Kuu ya Maendeleo ya Jamii.
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa Baraza hilo lililofanyika katika Makao ya Taifa ya Watoto Kikombno Jijini Dodoma.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW
**********************
Na Mwandishi Wetu Dodoma
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mwanaidi Ali Khamis amemuagiza Katibu Mkuu Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt John Jingu kutumia Wataalam wake kusimamia majukumu ya Wizara kuhakikisha watumishi wanafanya kazi kwa weledi.
Naibu Waziri Mwanaidi ametoa agizo hilo leo jijini Dodoma wakati akifungua Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Afya-Idara ya Maendeleo ya Jamii liliofanyika katika ukumbi wa Makao ya Taifa ya Watoto ya Kikombo.
Amesema kuwa Wizara ianatakiwa kuwatumia ipasavyo watumishi wake katika kuhakikisha mipango iliyowekwa inasimamiwa na kutekelezwa kikamilifu ili kuboresha huduma za Wizara hiyo na kutatua changamoto mbalimbali katika jamii.
Aidha, amewataka watendaji katika ngazi mbalimbali kuweka mkakati mbalimbali wa kutatuzi wa changamoto za jamii ikiwemo tatizo la ndoa za katika umri mdogo na vitendo vyote vya ukatili wa kijinsia.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Afya-Idara ya Maendeleo ya Jamii Dkt John Jingu amesema lengo la Baraza hilo la Wafanyakazi ni kushirikiana watumishi katika mipango na utekelezaji wa majukumu ya Wizara.
Dkt. Jingu amesisitza kuwa vikao vikao vya Baraza la wafanyakazi ni kiunganishi muhimu kinachoweza kuiwezesha Menejimenti na Watumishi kufanya kazi kwa weledi na kuondokana na dukuduku miongoni mwa wafanyakazi.
Ameongeza kuwa Baraza la Wafanyakazi likifanikiwa kufanya kazi zake vizuri, wafanyakazi watatimiza wajibu wao kwa kuzingatia maadili na weledi wa hali ya Juu.
Akizungumzia hoja mbalimbali zilizowasilishwa na Wajumbe wa Baraza, Dkt. Jingu amewataka wafanyakazi wa wenye hoja kuziwasilisha katika mamlaka ili ziweze kupata ufumbuzi.
“Pale penye hoja kama madeni na stahiki mbalimbali leteni, tufanye tuhakiki na kulipa madeni na stahili mbalimbali.” Alifafanua Dkt. Jingu.
Katika hatua nyingine, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Mwanaidi Ali Khamis amewatembelea watoto waishio katika makao ya Taifa ya kuelela watoto wenye mazingira magumu yaliyopo Kikombo Ddodoma na kutoa zawadi ikiwa ni kuelekea Siku Kuu ya Eid El Fitr.
Naibu Waziri huyo amesema Zawadi hiyo imetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ikiwa ni kuwawezesha Watoto hao kusherehekea Siku hiyo kwa furaha kama ilivyo kwa familia zingine.
Akizungumza mara baada ya kupokea zawadi hizo, Mkuu wa Makao hayo Tullo Masanja amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwakumbuka watoto hao katika kipindi cha Sikukuu na kuhakikisha kuwa Mkao hayo yataendelea kutoa huduma stahiki kwa watoto.