Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Zanzibar, Mhe. Haroun Ali Suleiman, akiwataka watakaopewa jukumu la kuendesha Boti iliyotolewa kwa Taasisi ya Mfuko wa Maendeleo ya Elimu Jimbo la Kikwajuni Zanzibar, kuwa waaminifu ili kutimiza lengo lililokusudiwa, wakati wa Mashindano ya saba ya Kuhidadhi Quran Viwanja vya Mao, Zanzibar.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango ambaye ni Mbunge wa jimbo la kikwajuni, Mhe. Mhandisi, Hamad Yussuf Masauni, akiwapongeza walioshiriki katika Mashindano ya Kuhifadhi Quran, yaliyofanyika katika Viwanja vya Mao, Zanzibar.
Mtoto Hasanati Khamis, akipokea zawadi ya Ushindi katika Mashindano ya Kuhifadhi Quran, yaliyofanyika katika Viwanja vya Mao Zanzibar, yakiwa ni mashindano ya Saba tangu yalipo asisiwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (wan ne kulia).
Mtoto Nahma, akiwa katika Mashindano ya Kuhidhi Quran, katika viwanja vya Mao Zanzibar, yeye akiwa amehifadhi Juzuu Moja.
Washindi wa Mashindano ya Saba ya Kuhifadhi Quran, yaliyofanyika katika Viwanja vya Mao Zanzibar, wakiwa wameshika zawadi zao zikiwemo fedha taslimu, baada ya kumalizika kwa mashindano hayo yaliyoanzishwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Zanzibar, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (hayupo pichani).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Zanzibar, Mhe. Haroun Ali Suleiman (wa pili kulia), akiongozwa na mwenyeji wake, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kikikwajuni, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (wa tatu kulia), katika Mashindano ya Kuhifadhi Quran, yaliyofanyika katika Viwanja vya Mao, Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Zanzibar, Mhe. Haroun Ali Suleiman (wa pili kushoto), akikabidhi Boti iliyotolewa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango ambaye ni Mbunge wa jimbo la kikwajuni, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (wa tatu kulia), kwa Taasisi ya Mfuko wa Maendeleo ya Elimu Jimbo la Kikwajuni, Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Zanzibar, Mhe. Haroun Ali Suleiman (katikati) na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (wa nne kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na Washindi wa Mashindano ya Quran, Jimbo la Kikwajuni, pamoja na viongozozi wengine katika Viwanja vya Mao, Zanzibar.
( Picha na Peter Haule, WFM, Zanzibar)
……………………………………………………………………………………
Na. Peter Haule, WFM, Zanzibar
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Zanzibar, Mhe. Haroun Ali Suleiman, amewataka watakaopewa jukumu la kuendesha Boti iliyotolewa kwa Taasisi ya Mfuko wa Maendeleo ya Elimu Jimbo la Kikwajuni kwa ajili shuguli za uchumi wa blue kuwa waaminifu ili kutimiza lengo lililokusudiwa.
Mhe. Waziri Suleimani ametoa rai hiyo kwa niaba ya Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi wa Shindano la Kuhifadhi Quran pamoja na kukabidhi Boti kwa Taasisi ya Mfuko wa Maendeleo ya elimu Jimbo la Kikwajuni, yaliyoandaliwa na kutolewa na Naibu Waziri Fedha na Mipango, na Mbunge wa jimbo hilo, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni.
Alisema kuwa bila kuwa na uaminifu katika matumizi ya Boti, hakuta kuwa na tija la boti hiyo, hivyo kudidimiza lengo la Taasisi ya Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo la kuwapatia ajira vijana kupitia Boti litakalotumika katika shughuli za uvuvi.
“Nimewahi toa Boti mbili tatu kwa ajili ya uvuvi lakini kila nikihitaji kupata mrejesho naambiwa leo baharini hakuingiliki au Samaki hawapatikani, wakati napata taarifa kwa wengine kuwa Samaki wamepatikana, kama hakutakuwa na vijana waaminifu basi mradi huo hautaendelea”, alieleza Mhe. Waziri Suleiman.
Aidha amewataka vijana kujiepusha na vitendo vya utumiaji dawa za kulevya, uzalilishaji na kukosa uaminifu ili miradi hiyo iliyobuniwa iweze kutekelezeka na kuwanufaisha vijana na Taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Fedha na Mipango ambaye ni Mbunge wa jimbo la kikwajuni, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni, amesema kuwa Serikali imekuwa ikiweka miundombunu wezeshi kwa wananchi, lakini kutokana na kukosekana kwa uaminifu miundombinu huharibiwa na miradi kufa, hivyo ameamua kutoa Boti kwa Taasisi Mfuko wa Maendeleo ya Elimu Kikwajuni ambayo inasimamiwa na watu wenye Imani ya Dini ili kukomesha ubadhirifu na kuleta tija stahiki.
Mheshimiwa Mhandisi Masauni amebainisha kuwa Boti na Mashine inathamani ya ya zaidi ya Shilingi milioni 15 na ameikabidhi Taasisi hiyo pamoja na Shilingi milioni tano ya mradi wa Majongoo Bahari, ili kutekeleza lengo la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar la kuwekeza nguvu kwenye uchumi wa Blue.
“Taasisi ya Mfuko wa Maendeleo ya Elimu Jimbo la Kikwajuni imekuwa na shughuli nyingi za kutatua changamoto za elimu kwa kufadhiliwa na watu binafsi kwa ruzuku, kwa kuwa Serikali inayonia thabiti ya kuhakikisha wananchi wanajikwamua kiuchumi, tumeamua kuifanya taasisi hiyo iweze kujiendesha kwa kiasi kikubwa kwa kutumia miradi yake yenyewe”, alieleza Mhandisi Masauni.
Kuhusu Mashindano ya Kuhifadhi Quran, yaliyofanyika katika Viwanja vya Mao Zanzibar, Mheshimiwa Mhandisi Masauni, aliwapongeza wote walioshiriki katika mashindano hayo ambayo lengo lake ni kuleta mshikamano na umoja miongoni mwa wananchi wa Jimbo la Kikwajuni na Wazanzibar kwa ujumla.
Alisema elimu ya Dini ni chachu kubwa katika kudumisha amani na uadilifu, hivyo ni muhimu mashindano haya yakaendelea kufanyika katika maeneo mbalimbali ili vijana waweze kukabiliana na changamoto ya utandawazi na mambo yasiyo na tija katika jamii
Amewapongeza vijana kwa kuonesha umahiri katika kuhifadhi Quran na kuwataka waendelee na juhudi hizo ili kuwa na kizazi chenye uaminifu si tu katika masuala ya Dini lakini pia katika shughuli za maendeleo ya nchi .