Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza Bungeni jijini Dodoma kuhusu maagizo ambayo ameyatoa kwa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, juu ya sakata la kuahirishwa kwa mechi ya Simba na Yanga ambayo ilipangwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Mkapa Dar es salaam, Mei 8, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
……………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesimama bungeni kuzungumzia tukio la kuahirishwa kwa mchezo wa watani wa jadi Simba na Yanga uliokuwa uchezwe Jumamosi, tarehe 8/05/2021.
Waziri Mkuu Majaliwa ametoa maagiza Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
kutoa taarifa haraka sana kwa Watanzania juu ya tarehe ya kuchezwa kwa mchezo huo na pia ieleze utaratibu kuhusu hatima ya waliolipa viingilio ili kushuhudia mchezo huo.
”Niwasihi Watanzania kuwa wavumulivu ili kuipa muda Wizara kwa kushirikiana na taasisi zinazosimamia mpira wa miguu ikiwemo TFF kuja na taarifa juu ya hatima ya mchezo huo”amesema
Mchezo wa Simba na Yanga ulipangwa kufanyika Mei 8,2021katika uwanja wa Benjamin Mkapa uliahirishwa kutokana na mabadiliko ya muda wa awali ambao ulipangwa kuwa saa 11:00 jioni lakini kabla muda huo kufika, TFF litoa taarifa ya kubadili muda mpaka saa 1:00 usiku.