Meneja Mkuu wa Boomplay Tanzania, Natasha Stambuli (kulia) akikabidhi msaada wa vifaa tiba kwa Muuguzi Kiongozi Idara ya nje ya Hospitali ya Mwananyamala, Pendaeli Massay (mwenye gauni la bluu). Msaada huo ulitolewa jana jijini Dar es Salaam ambapo Boomplay waliadhimisha Siku ya kina mama duniani kwa kutoa vifaa vya matibabu kwa Hospitali ya Mwananyamala, kuunga mkono juhudi za hospitali hiyo za afya salama na ya uhakika kwa akina mama nchini.
Meneja Mkuu wa Boomplay Tanzania, Natasha Stambuli (kulia) akikabidhi msaada wa vifaa tiba kwa Muuguzi Kiongozi Idara ya nje ya Hospitali ya Mwananyamala, Henrietta Ishara (wa tano kulia). Msaada huo ulitolewa jana jijini Dar es Salaam ambapo Boomplay waliadhimisha Siku ya kina mama duniani kwa kutoa vifaa vya matibabu kwa Hospitali ya Mwananyamala, kuunga mkono juhudi za hospitali hiyo za afya salama na ya uhakika kwa akina mama nchini.
Meneja Mkuu wa Boomplay Tanzania, Natasha Stambuli (kulia) akiwashukuru wauguzi wa hospitali ya Mwananyamala mara baada ya kukabidhi msaada wa vifaa tiba katika hospitali hiyo jana jijini Dar es Salaam. Boomplay waliadhimisha siku ya kina mama duniani kwa kutoa vifaa vya matibabu katika hospitali hiyo, kuunga mkono juhudi za afya salama na ya uhakika kwa akina mama nchini.
***********************
Dar es Salaam. Boomplay, App inayoongoza barani Afrika kwa huduma ya kusikiliza na kupakua muziki imeadhimisha Siku ya kina mama mwaka huu kwa kutoa vifaa vya matibabu kwa Hospitali ya Mwananyamala, kuunga mkono juhudi za hospitali hiyo za afya salama na ya uhakika kwa akina mama nchini.
Hospitali hiyo, ambayo ni hospitali Kuu ya Rufaa jijini Dar es Salaam inahudumia wastani wa akina mama wajawazito 900-1,400 kila mwezi.
Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika eneo la hospitali siku ya Jumapili, Meneja Mkuu wa Boomplay Tanzania, Natasha Stambuli alisema msaada huo ni sehemu ya utekelezaji wa mipango endelevu inayolenga kusaidia jamii.
“Tunayo furaha kutumikia jamii yetu na hasa katika siku hii ya akina Mama duniani. Tunaelewa mchango na shida wanazopitia akina mama hasa wakati wa uzazi katika jamii zetu.
Tunapowasherehekea kina mama, tunafurahi kuchangia msaada wetu na tunatarajia kufanya mengi zaidi kwenye jamii katika siku usoni, “alisema Bi Stambuli.
Hamasa hiyo iliungwa mkono na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mwananyamala, Dkt. Zavery Benela, ambaye aliisifu Kampuni hiyo kwa msaada wake, na kuongeza kuwa umekuja katika muda muafaka wakati ambao Ulimwengu unakabiliwa na changamoto ya huduma ya afya.
“Kwa niaba ya hospitali nzima, ningependa kutoa shukrani zangu za dhati kwa Boomplay kwa msaada huu wa huruma. Tuna hakika kuwa mchango wao utasaidia sana katika kuhakikisha huduma zetu za kina mama zinaendelea bila kukatizwa”.Alisema Dkt. Zavery Benela.
“Ninahimiza Kampuni na wadau wengine kuiga ishara hii nzuri, ili kutimiza juhudi zetu katika kuhakikisha kuwa akina mama na watoto wao wachanga wanapata huduma na matibabu ya hali ya juu”.Alisema.
Mpango huo ni mwanzo wa miradi mingine mingi ya jamii ambayo Boomplay inakusudia kuzindua katika siku za usoni.
“Kama kampuni, tunaendelea kujitolea kutekeleza jukumu letu katika jamii, kwa lengo la kuleta matokeo chanya na kuacha alama katika maisha ya wengi,” Bi Stambuli alimalizia.