Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahenge akizungumza wakati wa mkutano na wananchi wa Kata ya Nkuhungu alipokuwa akipokea ripoti ya kamati aliyoiunda kutathmini athari za mafuriko katika mitaa ya Bochela, usalama, Mnyakongo na Mtube ambapo serikali imewatafutia viwanja vingine takribani 500 waathirika hao.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahenge akionyesha karatasi yenye majina ya watu wanaostahili kupata viwanja wakati wa mkutano na wananchi wa Kata ya Nkuhungu alipokuwa akipokea ripoti ya kamati aliyoiunda kutathmini athari za mafuriko katika mitaa ya Bochela, usalama, Mnyakongo na Mtube ambapo serikali imewatafutia viwanja vingine takribani 500 waathirika hao.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Josephat Maganga akizungumza wakati wa mkutano wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na wananchi wa Kata ya Nkuhungu alipokuwa akipokea ripoti ya kamati aliyoiunda kutathmini athari za mafuriko katika mitaa ya Bochela, usalama, Mnyakongo na Mtube ambapo serikali imewatafutia viwanja vingine takribani 500 waathirika hao.
Mbunge wa Dodoma Mjini Mhe. Antony Mavunde akizungumza wakati wa mkutano wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na wananchi wa Kata ya Nkuhungu alipokuwa akipokea ripoti ya kamati aliyoiunda kutathmini athari za mafuriko katika mitaa ya Bochela, usalama, Mnyakongo na Mtube ambapo serikali imewatafutia viwanja vingine takribani 500 waathirika hao.
Mwenyekiti wa Kamati iliyokuwa ikitathmini athari katika eneo hilo bw. Michael Maganga akizungumza wakati wa mkutano wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na wananchi wa Kata ya Nkuhungu alipokuwa akipokea ripoti ya kamati aliyoiunda kutathmini athari za mafuriko katika mitaa ya Bochela, usalama, Mnyakongo na Mtube ambapo serikali imewatafutia viwanja vingine takribani 500 waathirika hao.
Mmoja wa wananchi waathirika wa mafuriko hayo bw. Poul Yohana akizungumza wakati wa mkutano wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na wananchi wa Kata ya Nkuhungu alipokuwa akipokea ripoti ya kamati aliyoiunda kutathmini athari za mafuriko katika mitaa ya Bochela, usalama, Mnyakongo na Mtube ambapo serikali imewatafutia viwanja vingine takribani 500 waathirika hao.
Baadhi ya nyumba ambazo kwa muda mrefu zikiwa zimezungukwa na maji mara baada ya mafuriko ambapo sasa ni msimu wa pili sasa wa mvua nyumba hizo zimezungukwa na maji na wakazi wake kukosa sehemu ya kuishi.
………………………………………………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
Serikali imetoa viwanja mbadala kwa wananchi wa mitaa ya Bochela, usalama, Mtube na Mnyakongo, ambao ni sawa na kaya 556 walioathirika na mafuriko kwa muda mrefu katika eneo la Nkuhungu Jijini Dodoma huku Serikali ikifanya jitihada za kuondoa maji katika eneo hilo ili waweze kurudi katika maeneo yao.
Uamuzi huo wa serikali umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahenge wakati wa mkutano na wananchi wa mitaa hiyo mara baada ya kupokea ripoti ya kamati aliyoiunda kwa ajiri ya kutathmini athari za mafuriko hayo ambapo amesema wananchi hao watapewa viwanja mbadala bure vyenye thamani za zaidi ya bilioni 2.3 wakati jitihada za kuondoa maji hayo zikiendelea.
“Wananchi hawa ambao serikali inawajali na haipendi wateseke, kwa sasa itawapa viwanja mbadala zaidi ya 500 bure kwa ajili ya kujenga nyumba zao katika maeneo ya Nala, Mahomanyika. kwani maji hayo ili kuondoa kwenye bwawa hilo zinahitajika takribani sh bilioni 9.6 kwa kutumia maboza 138 388 yenye matengi ya ujazo wa lita 10,000 kila moja, viwanja vya hapa vitabaki kuwa vyenu,” amesema Dkt Mahenge.
Ameongeza kuwa “Maji haya yaliyojaa tangu ilipoanza mvua za masika Desemba mwaka jana yameunda bwawa linalofikia mita za ujazo 1,383,878 sawa na lita 1,383,878,000 ambazo zinaweza kutumika hapa jijini kwa siku 13” amesema.
Dk Mahenge amesema mkakati wa serikali kutafuta fedha ili kupata suluhisho la kudumu kwa kujenga mitaro miwili badala ya kuondoa maji katika eneo hilo kwani kutumia maboza ambako ni gharama kubwa na itatakiwa kufanya hivyo kila msimu wa mvua kila mwaka.
“Fedha zikipatikana serikali itajenga mitaro miwili mikubwa kwa gharama ya Sh milioni 1.319, ambapo mmoja unaotiririsha maji kutoka kwenye mabwawa na mwingine utakaokinga maji ya mtiririko pembezoni mwa barabara kuu ya Dodoma – Singida na kuyapeleka kuungana na mtaro wa asili wa mailimbili ambayo itafunikwa na kesho nakutana na waziri Mkuu kuzungumza hili.” Amesema.
Katika kuhakikisha maji hayo yanapungua wakati serikali ikifanya jitihada za kuondoa maji hayo ameagiza katika kazi zote za ujenzi zinazoendelea maeneo mengi katika jiji la Dodoma ameelekeza maji yachukuliwe katika eneo hilo ili kusaidia kupungua kwa maji hayo.
Awali akiwasilisha ripoti ya Kikosi Kazi kilichoundwa na Mkuu wa Mkoa kuchunguza changamoto hiyo bwana Michael Maganga amesema halmashauri ya jiji la Dodoma inatakiwa kutangaza kwamba eneo hilo lenye ukubwa wa ekari 147 ni eneo hatarishi na halifai kwa makazi ya binadamu, linatakiwa kuzungushiwa uzio katika eneo la upana wa mita 60.
Amebainisha kuwa kwa sasa jiji hilo linatakiwa kusitisha shughuli za kibinadamu katika eneo hilo kama uvuvi, kilimo na matumizi mengine ya nyumbani ya maji ili kuzuia magonjwa ya mlipuko yanayoweza kujitokeza kwa wananchi kwa kuwa maji hayo yamekaa kwa muda mrefu pia kuchangamana na maji taka.
Baadhi ya wananchi ambao walikuwepo katika kikao hicho wameishauri serikali kuharakisha katika kuyatoa maji hayo kwani baadhi yao hawana uwezo wa kujenga katika maeneo mengine kwani kipato chao ni kidogo, hivyo wanategemea eneo hilo huku wengine wakidai kuna baadhi ya viwanja vilirukwa wakati wa tathmini hiyo hasa kwa nyumba zilizokuwa hatua ya chini na viwanja.
Naye Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa uamuzi huo kwani wananchi hao wameteseka kwa muda mrefu lakini kwa sasa wamepata matumaini tena kwa kupata viwanja vingine.