Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul (kulia) akizungumza Mei 08, 2021 Jijini Mbeya wakati Mhe. Tulia Ackson (hayupo pichani) Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipofika Shule ya Sekondari Lioto ya Jijini hapo kufungua Chumba cha Kompyuta pamoja na Ofisi ya walimu kupitia taasisi yake yake ya Tulia Trust Fund.Kushoto ni baadhi ya Manaibu Mawaziri pamoja na Wabunge waliohudhuria tukio hilo.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul (kushoto) akijadiliana jambo na Mhe. Tulia Ackson Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walipofika Shule ya Sekondari Lioto ya Jijini hapo kufungua Chumba cha Kompyuta pamoja na Ofisi ya walimu kupitia taasisi yake yake ya Tulia Trust Fund.Kushoto.Kushoto ni Naibu Waziri wa Maji Mhe.MaryPrisca Mahundi.
Mhe. Tulia Ackson Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akizungumza Mei 08,2021 Jijini hapo kuhusu Marathon iliyofanyika iliyokua na lengo la kuboresha Miundombinu ya Elimu na Afya.Kushoto ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul pamoja na Waheshimwa Wabunge.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul akiwa katika picha ya pamoja na Washindi wa KM 21 Wanaume ambao ni Alphonce Simbu,Emmanuel Giniki na Joseph Panga pamoja na viongozi wao baada ya kushiriki Mbio za Tulia Marathon zilizofanyika Mei 08,2021 Jijini Mbeya kwa udhamini wa Mhe. Tulia Ackson (hayupo pichani) Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza wa KM 42 Wanawake Bi.Monica Cheluto kutoka Kenya katika mbio za Tulia Marathon zinazodhaminiwa na Mhe. Tulia Ackson Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zilizofanyika Mei 08, 2021 Jijini Mbeya.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza wa KM 42 Wanaume Hamis Athuman katika mbio za Tulia Marathon zinazodhaminiwa na Mhe. Tulia Ackson Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zilizofanyika Mei 08, 2021 Jijini Mbeya.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul akimpokea zawadi ya picha yake iliyochorwa na msanii kutoka Jijini Mbeya baada ya kumalizika kwa mbio za Tulia Marathon zinazodhaminiwa na Mhe. Tulia Ackson Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zilizofanyika Mei 08, 2021 Jijini Mbeya.Kushoto ni Mtangazaji Millard Ayo.
Mhe. Tulia Ackson Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akimalizia mbio za KM 05 katika mbio za Tulia Marathon zilizofanyika Mei 08, 2021 Jijini humo.
Mhe Rose Tweve (Mbunge) akiwa ameshika nafasi ya kwanza katika Mbio za Mita 100 kwa upande wa Wabunge Wanawake ikiwa ni sehemu ya Mbio za Tulia Marathon zinazodhaminiwa na Mhe. Tulia Ackson Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zilizofanyika Mei 08, 2021 Jijini humo.
Mhe Stansilaus Mabula (Mbunge) akiwa ameshika nafasi ya kwanza katika Mbio za Mita 100 kwa upande wa Wabunge Wanaume ikiwa ni sehemu ya Mbio za Tulia Marathon zinazodhaminiwa na Mhe. Tulia Ackson Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zilizofanyika Mei 08, 2021 Jijini humo.
………………………………………………………………………..
Na Shamimu Nyaki-WHUSM,Mbeya
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Pauline Gekul amezitaka Halmashauri zote nchini kusimamia michezo kuanzia ngazi za vijiji ili wananchi waweze kuimarisha afya zao na kukuza michezo kuanzia ngazi ya chini hadi Taifa.
Mhe. Gekul ametoa maagizo hayo Mei 08, 2021 Jijijini Mbeya akiwa Mgeni Rasmi katika Mbio za Tulia Marathon zinazodhaminiwa na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson.
“Nafahamu kuna asilimia 40 inayotengwa na Halmashauri kwa ajili ya shughuli za maendeleo, natoa rai kwa viongozi wa Halmashauri kutenga fedha kidogo kwenye hiyo asilimia ambazo zitawezesha shughuli za michezo kwenye maeneo yenu kuanzia ngazi za chini kabisa kwenye vitongoji”, amesisitiza Mhe. Gekul.
Kwa upande wake, Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson amesema lengo la mashindano hayo ni kuboresha Miondombinu ya Elimu na Afya kupitia Taasisi ya TuliaTrust Fund kwenye Jimbo hilo ambapo zinatarajiwa kufikia Watanzania wengi hapo baadae.
“Tulia Trust Fund ipo kwa ajili ya kusadia na kuwezesha wananchi kiuchumi,tangu mwaka 2018 taasisi hii imesadia wananchi kupitia miradi mbalimbali ikiwemo kuboresha madarasa, mabweni na upatikanaji wa maji na kazi inaendelea” amesema Mhe.Tulia
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Riadha Nchini Filbert Bay amempongeza Naibu Spika huyo kwa kuanzisha mashindano hayo ya riadha.
Mbio hizo zinajumuisha mbio za ndani na nje ya uwanja ambapo kwa hapa nchini zimefanyika kwa mara ya kwanza.
Naye Mshiriki aliyeshika nafasi ya tatu katika mbio za KM 21 ambaye pia ni miongoni mwa Timu ya Taifa ya Riadha inayowakilisha nchi katika mashindano ya Riadha yatakayofanyika baadae mwaka huu nchini Japan, Bw. Alphonce Simbu amesema mashindano hayo yamemsadia kufanya mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya mashindano yajayo ya Kimataifa ambapo ameahidi kufanya vizuri na kuitangaza nchi.
Mbio hizo hufanyika kila mwaka ambapo kwa mwaka huu zimegawanyika katika makundi ya KM 42 na 21 kwa wanaume na wanawake, Mbio za ndani ya Uwanja kwa Mita 100, 200, 400, 800 na 1500 ambapo pia Viongozi na Waheshimwa Wabunge wameshiriki.