TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TUME YA UTUMISHI WA UMMA KUTOA MAFUNZO KWA WATUMISHI WA KADCO
Tume ya Utumishi wa
Umma inatarajia kutoa mafunzo kwa
Watumishi wa Kampuni ya Uendelezaji wa Kiwanja cha Ndege Kilimanjaro (KADCO)
Mkoani Kilimanjaro.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jijini Dar es Salaam na Katibu wa Tume ya
Utumishi wa Umma, Bwana Nyakimura Muhoji amesema kuwa mafunzo haya yameandaliwa
na KADCO kwa lengo la kuwajengea uwezo Watumishi wa KADCO kuhusu Utekelezaji wa
Sheria ya Utumishi wa Umma Sura 298 na Usimamizi wa Utendaji Kazi kupitia Mfumo
wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji kazi (OPRAS), kuwawezesha kutekeleza
majukumu yao kwa kuzingatia Sheria, Kanuni,
Taratibu na Miongozo inayosimamia masuala ya Rasilimali Watu katika Utumishi wa
Umma.
Mafunzo
haya ya wiki mbili yatafanyika kuanzia
siku ya Jumatatu tarehe 10 Mei, 2021 na yatafunguliwa Rasmi na Kamishna wa Tume
ya Utumishi wa Umma, Mheshimiwa George D. Yambesi kwa niaba ya Mwenyekiti wa
Tume ya Utumishi wa Umma, Mheshimiwa Jaji (Mstaafu) Dkt. Steven J. Bwana na
yatahitimishwa tarehe 24 Mei, 2021.
Bwana
Muhoji amesema, Tume inatekeleza jukumu hili
kwa mujibu wa Kifungu cha 10 (1) ( C) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Sura 298.
Imetolewa
na:-
Kitengo cha
Mawasiliano Serikalini
TUME YA UTUMISHI WA
UMMA
DAR ES SALAAM
07 Mei, 2021