************************
JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAWASHIKILIA WATUHUMIWA KUMI (10) WA MAKOSA MBALIMBALI YA KIUHALIFU.
TUKIO LA KWANZA; KUHUJUMU MIUNDOMBINU YA DARAJA KIGONGO –BUSISI.
TAREHE 04/05/2021 MAJIRA YA SAA 05:00 HRS HUKO MAENEO YA KILABELA, BARABARA YA BUSISI- GEITA, WILAYA YA SENGEREMA, MKOA WA MWANZA, JESHI LA POLISI LILIWAKAMATA WATUHUMIWA NANE (8) KWA KOSA LA KUHUJUMU MIUNDOMBINU YA UJENZI WA DARAJA LA KIGONGO- BUSISI (WIZI WA VIFAA), AMBAPO WALIKAMATWA WAKIWA NA GARI LENYE NAMBA T.610 DNV AINA YA TOYOTA HIACE LILILOKUWA LIMEBEBA VIFAA VYA UJENZI VILIVYOIBIWA AMBAVYO NI H. BEAM 19, BOLT KUBWA 16, CUTTING TOT/WELDING BUBRO 03,GAS PIP 02 NA CABLE WIRE 01 NYEUSI.
AIDHA KATIKA MAHOJIANO YA AWALI DEREVA WA GARI HILO ALIELEZA KUWA VIFAA HIVYO ALIPEWA NA JOSHUA WILSON, MIAKA 43, MZINZA, FUNDI WA KUCHOMELEA VYUMA /WELDER WA MBUGANI, AMBAYE NAE ALIPOHOJIWA ALIELEZA KUWA AMEVINUNUA KWA MAFUNDI WATATU WA MRADI HUO WA DARAJA LA KIGONGO -BUSISI LINALOENDELEA KUJENGWA. WATUHUMIWA WOTE WAMEKAMATWA, JESHI LA POLISI LINAENDELEA NA UCHUNGUZI WA KINA, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA WATUHUMIWA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI.
JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINATOA ONYO KWA MAFUNDI UJENZI WA DARAJA HILO KUACHA MARA MOJA TABIA YA KUIBA VIFAA VYA UJENZI, KWANI HATA WAKIIBA MSUMARI MMOJA NI KOSA KISHERIA NA TUTAWASHUGHULIKIA VIKALI KWA MUJIBU WA SHERIA.
TUKIO LA PILI; KUJERUHI.
TAREHE 05.05.2021 MAJIRA YA SAA 20:00 HUKO KIJIJI/KATA/ TARAFA NA WILAYA YA MISUNGWI, ANCELEMI MUSSA, MIAKA 19, MJITA, MWANAFUNZI WA CHUO CHA VETA- KAHAMA ALIJERUHIWA KWA KUCHOMWA NA KITU CHENYE NCHA KALI (KISU) MAENEO YA MGONGONI NA ALFRED EMANUEL, MIAKA 16, MSUKUMA, MKULIMA NA MKAZI WA MAJENGO KANISANI NA KUMSABABISHIA MAUMIVU MAKALI MWILINI, HII NI BAADA YA MGOGORO WA KUDAIANA FEDHA KIASI CHA TSH 15,000/=. MAJERUHI AMELAZWA HOSPITALI YA WILAYA YA MISUNGWI KWA MATIBABU.
PIA, TAREHE 05.05.2021 MAJIRA YA SAA20:45 HUKO KATIKA KIJIJI/ KATA YA NAKATUNGURU, WILAYA YA UKEREWE, GETRUDA MAFOLO, MIAKA 69, MJITA, MKRISTO, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA NAKATUNGURU, AKIWA NYUMBANI KWAKE ALIJERUHIWA KWA KUCHOMWA NA KISU MGONGONI NA PILI MAKURU, MIAKA 28,MKURYA,MKAZI WA KIJIJI CHA NAKATUNGURU NA BAADAE NA YEYE KUJICHOMA NA KISU UBAVUNI UPANDE WA KUSHOTO. MAJERUHI WAMELAZWA HOSPITALI YA WILAYA YA UKEREWE NA HALI ZAO SIO NZURI.
JESHI LA POLISI LINATOA ONYO KALI KWA WANANCHI KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI PINDI WANAPOKUA KWENYE MIGOGORO BALI WAFUATE SHERIA NA TARATIBU ZILIZOWEKWA ILI KUEPUSHA VIFO NA MAJERUHI.
TUKIO LA TATU. MTOTO KUUAWA NA MNYAMA WA PORINI/FISI
TAREHE 06/05/2021 MAJIRA YA SAA 19:30 HUKO KITONGOJI CHA NYAMUGE, KIJIJI CHA KITONGO, KATA YA KITONGOSIMA, WILAYA YA MAGU , MTOTO AITWAYE DAUDI MUSSA, MIAKA 03, MKRISTO, MKAZI WA KITONGOJI CHA NYAMUGE, ALIUAWA KWA KULIWA NA FISI AKIWA ANACHEZA JIRANI NA NYUMBANI KWAO.
AIDHA WAKATI WA TUKIO MAMA MZAZI WA MAREHEMU ALIKUWA NDANI ANAPIKA GHAFLA ALIONA MTOTO ANAKOKOTWA NA FISI NDIPO ALIPIGA YOWE KUOMBA MSAADA KWA MAJIRANI, WANANCHI WALIANZA KUFUATILIA MICHIRIZI YA DAMU HADI MLIMANI NA KUKUTA MTOTO AMEFARIKI DUNIA
.
JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAWAOMBA WANANCHI KUWA MAKINI NA WATOTO WANAPOKUA WANACHEZA DHIDI YA WANYAMA WAKALI, PIA JESHI LA POLISI LINAENDELEA NA MSAKO MKALI KWA KUSHIRIKIANA NA JESHI LA WANYAMAPORI KUHAKIKISHA FISI HUYO ANAKAMATWA ILI ASIENDELEE KULETA MADHARA KWA WANANCHI.