Balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe. Dkt John Steven Simbachawene akizungumza na watendaji na wataalamu kutoka Tanzania waliokuwa nchini Kenya kwa ajili ya kuhakikisha ziara ya Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan nchini Kenya inafanyika kwa mafanikio
Watendaji na wataalamu kutoka Tanzania ambao walikuwa nchini Kenya kwa ajili ya kufanikisha ziara ya Mhe. Rais alipoitembelea Kenya tarehe 4-5 Mei 2021 wakiwa katika ukumbi wa mikutano katika Ubalozi wa Tanzania jijini Nairobi.
Balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe. Dkt John Simbachawene (katikati) akiwa na Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) Bw. Maduhu Kazi (wa kwanza kushoto), Mkurugenzi wa Mamlaka ya maeneo Maalum ya Mauzo ya Nje (EPZA) (wa kwanza kulia), Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Bw. Edwin Rutageruka (wa pili kulia), na Mkurugenzi Mkuu wa Shirka la Viwango Tanzania (TBS) Dkt. Yusuf Mngenya (wa pili kushoto) walipokutana kwa mazungumzo ofisini kwa Mhe. Balozi jijini Nairobi.
Balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe. Dkt John Steven Simbachawene (katikati) akiwa na Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) Bw. Maduhu Kazi (wa kwanza kushoto), Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Mauzo ya Nje (EPZA) Bw. (wa kwanza kulia), Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Bw. Edwin Rutageruka (wa pili kulia), na Mkurugenzi Mkuu wa Shirka la Viwango Tanzania (TBS) Dkt. Yusuf Mngenya (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika Wizara ya Mambo ya Nje Bw. Frank Mwega na maafisa Ubalozi walipokutana kwa mazungumzo ofisini kwa Mhe. Balozi jijini Nairobi.
Balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe. Dkt. John Simbachawene katika picha ya pamoja na watendaji kutoka Tanzania waliofanikisha ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliyoifanya nchini Kenya tarehe 4-5 Mei 2021.
******************************
Balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe. Dkt. John Simbachawene ameipongeza timu ya watendaji na wataalamu kutoka Tanzania kwa kufanikisha ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliyoifanya nchini Kenya tarehe 4-5 Mei 2021.
Dkt. Simbachawene ametoa pongezi hizo katika Ubalozi wa Tanzania jijini Nairobi alipokutana na timu ya watendaji na wataalamu kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Wizara ya Viwanda na Biashara.
“Nawashukuru na kuwapongeza kwa kazi kubwa na nzuri mliyoifanya hadi kukamilika kwa ziara ya Mhe. Rais, ni wazi kuwa kufanya kazi kwa pamoja ni kitu kizuri wote tumeona hapa, asanteni sana na hongereni kwa kazi,” alisema Dkt. Simbachawene.
Amewataka watendaji hao kuhakikisha wanazingatia na kutekeleza yale yote yaliyoongelewa na kutolewa maelekezo na viongozi wakuu wa nchi hizi ili kuhakikisha vikwazo vya biashara visivyo vya kodi vinaondolewa na hvyo kukuza na kuimarisha uwekezaji na biashara kwa manufaa ya nchi zote mbili.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alifanya ziara ya kikazi ya siku mbili nchini Kenya kwa mwaliko wa mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta. Ziara hiyo ilifanyika tarehe 4-5 Mei 2021 na kushuhudia makubaliano kati ya Tanzania na Kenya kuhusu kushirikiana kwenye masuala ya utamaduni na ujenzi wa bomba la gesi asilia kutoka Dar es Salaam hadi Mombasa yakisainiwa kwa ajili ya utekelezaji
Katika ziara hiyo Viongozi wa nchi hizo walikubaliana kuondoa vikwazo vya biashara vilivyopo baina ya nchi hizo vinavyozuia uwekezaji na biashara katika nchi hizo na hivyo kushindwa kukuza uchumi wa nchi hizo .